Tuesday, 26 April 2011

Ajali ya boti yaua 38 Ziwa Kivu

Low cloud descends on Kashmiri boatmen as they row their boats during heavy rain at Dal Lake in Srinagar 01, April  2011.

http://youtu.be/81y3tR_xpS0
embu tizama hiyo video kwenye link uone kwenye boti hiyo kama kuna usalama

Kivuko kimoja kimezama katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuua watu wasiopungua 38, kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu.
Inaaminika chombo hicho kilikabiliwa na upepo mkali na mawimbi baada ya kutoka Minova kikiwa njiani kwenda mji wa Bukavu siku ya Jumapili jioni.
Kikosi cha uokoaji cha Msalaba Mwekundu kimefanikiwa kuokoa watu 11 na abiria wengine 50 bado hawajapatikana.
Mashua ni usafiri unaotumika sana huko Kongo-Kinshasa, ambayo haina barabara za kutosha wala njia za reli lakini imejaliwa maziwa na mito.
Desire Yuma, rais wa Msalaba Mwekundu jimbo la Kivu Kusini, amesema jitihada za uokoaji zitaendelea mpaka Jumanne asubuhi.
Kwa mujibu wa Msalaba Mwekundu na mfanyakazi wa shirika moja la usafiri wa majini maeneo hayo, chombo kilichopata ajali ni cha wazi, kilichoundwa kwa mbao kikiwa na mota, na kilikuwa kimebeba mizigo na abiria takriban 100.
Mwandishi wa BBC, Thomas Hubert aliyeko katika mji mkuu Kinshasa, amesema janga hilo ni kielelezo kingine kuhusu usalama duni kwenye vyombo vya usafiri wa majini vinavyotumika katika mito na maziwa ya nchi hiyo.
Mara kwa mara serikali huwalaumu wamiliki wa vyombo hivyo kwa kupuuza sheria za usafirishaji na kubeba mizigo na abiria kupita kiasi, ameeleza.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment