Monday, 4 April 2011

UN-Mauaji ya Ivory Coast yanaogofya

Troops loyal to Alassane Ouattara head to Abidjan (3 April 2011)

katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea mshtuko wake kufuatia taarifa za mauaji ya mamia ya watu mjini Duekoue magahribi mwa Ivory Coast.
Ban Ki Moon amemtaka Alassane Ouattarra anayetambuliwa na jamii ya kimataifa kama mshindi wa kura za Urais nchini humo, afanye uchunguzi kufuatia tetesi kuwa wafuasi wake wanahusika na mauaji hayo.
Bw Ouattarra hata hivyo amekanusha madai kuwa wapiganaji wanaomuunga mkono wanahusika na kisa hicho.
Taarifa za awali za Umoja wa Mataifa zinasema watu 330 waliuawa.
Vikosi vya kulinda usalama vya Umoja huo sasa vinawalinda maelfu ya watu waliokimbilia hifadhi katika kanisa moja mjini Abidjan baada ya mapigano kuchacha.
Wakaazi mjini humo wanasema hali imetulia kwa sasa lakini kuna amri ya kutotoka nje ambayo inatekelezwa.
Wapiganaji wanaomuunga mkono Bw Ouattarra wamefaulu kudhibiti maeneo mengi nchini humo tangu mashambulizi dhidi ya Gbagbo na wafuasi wake yaanze wiki iliopita.
Taarifa zinasema kuwa mkuu wa majeshi Philippe Mangou, ambaye alitangaza kujiunga na Bw Ouattarra wiki iliopita, ametoka kwenye ubalozi wa Afrika Kusini alipoomba hifadhi.
Jenerali Mangou sasa amekubali kurejelea majukumu yake baada ya kufanya mazungumzo na Laurent Gbagbo.
Taarifa zingine zinasema kuwa Umoja wa Mataifa unapanga kuwahamisha wafanyikazi wake 200 walioko mjini Abidjan.

BBC.

No comments:

Post a Comment