bajaj ambulance
bajaj zimamoto
mara nyingine huwa nahisi kama naota vile nikiona mizaha mizaha kama hii,mwanzoni walianza na bajaj ambulance kama utani,tukapiga kelele wee aah wapi tumeonekana wajinga tu tunaongea na kompyuta wala hatujui lolote ikapitishwa.
na sasa wamekuja na idea mpya bajaj za kuzima moto!huwezi kuamini katika karne hii nchi nyingine wanapiga hatua zaidi kiteknolojia na kisayansi sisi ndio kwanza tuko kwenye "mark time na nyumaa geuka"
ok wengine watasema si afadhali wanaleta bajaj kwani ni kweli watu wanapakiwa kwenye mikokoteni na baiskeli huko vijijini,lakini je bajaj ndio uvumbuzi kweli??,nashindwa kuelewa kwamba viongozi baada ya kukaa kwa muda mrefu na ahadi tele za maisha bora miaka yooote hatimaye kutimiza ahadi wamenunua bajaj za kubeba wagonjwa!.
bajaj hizi kwetu kule kwenye milima ya uporoto itapanda milima saa ngapi zaidi ya kurudi kinyumenyume na kumtupa mgonjwa makorongoni?tunawatakia mema hawa wagonjwa kweli??
haya sisi tunapiga kelele lakini tenda inapitishwa na wanasiasa wanakula chao cha juu ishazoeleka hiyo,wahenga walisema ukila nyama ya mtu hutaacha kula hiyo ndio ufisadi ulivyo sasa,hata mahali pasipotakiwa ufisadi viongozi wanalazimisha almradi tu wapate kula yao basi.
balaa sasa ukiambiwa hiyo bajaj moja ya wagonjwa bei yake ni sawa na ambulance hiace mbili waweza tukana matusi yoote unayoyajua lakini ndio hivyo tushaliwa na wakubwa wamepitisha na bajaj 400 ambulance zitatua bongo ambazo thamani yake ni sawa na toyota hiace ambulance zaidi ya 600,hapo ndio tutachoka.
sasa bado wakati tukijiuliza maswali yasiyo majibu kuhusu hizo bajaj ambulance sasa wametujia na idea nyingine bajaj ya fire,hivi hicho kibajaj hapo kinabeba galoni ngapi za maji?huto tumaji kweli waweza zima nato moto kweli??
mara ngapi tushaona magari yenyewe yale makubwa ya fire yanaenda zima moto na mpaka maji yanaisha kwenye tanki na nyumba inaungua mpaka jivu.sasa leo iwe kibajaj na vigalon vya maji,kwanza kwa usalama jinsi maji yanavyocheza cheza ndani ya gari ikitembea unategemea hicho kibajaj kitafika kweli kikiwa na mzigo wa maji? na kitaenda kwa spidi gani wakati nyumba inaungua?
haya maswali yoote sipati majibu zaidi ya kizunguzungu,lakini aah ishapita hiyo na waziri mkuu"mtoto wa mkulima" kashazindua hiyo iliyobaki vibajaj vitaingia toka india mradi wa ponjoro mmoja na tenda itapitishwa fisadi mmoja atakula ten percent yake maisha yanaendelea.
ndio tunavyoishi.sina mengi ninasikia machungu na nchi yangu ila basi tu ndo wao wameshika mpini.
"mafisadi tunaomba mutuonee huruma wajameni ili siku ya mabadiliko na sisi tuwaonee japo huruma yasiwakute ya gbagbo."
nyie haya tu tutaonana siku yenu ikifika hata miaka mia ipite.
No comments:
Post a Comment