Tuesday, 26 April 2011

LEO TUNAADHIMISHA MIAKA 47 YA MUUNGANO


siku kama ya leo miaka 47 iliyopita ndio udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa na kuwa kitu kimoja na ndipo ilipozaliwa TANZANIA.
baada ya miaka hii 47 sasa asilimia kubwa ya wazanzibari hawautaki muungano.wanasema kwamba sasa imekuwa kama wametawaliwa na wabara,hivyo wanahitaji kujitenga wapewe nchi yao ya zanzibar na wawe huru kujiunga na nchi yoyote(hasa oman) lakini siyo Tanganyika.
inawezekana kilio chao ni sahihi si cha kudharau lakini je kitakubalika??

kwa namna hali ilivyo sasa hapo nyumbani ni haki ya wazanzibar kudai haki yao ya kuvunjwa muungano,wenzetu wanaona mbali na umasikini huu wa wananchi,katika miaka yote zaidi ya 50 ya uhuru hamna faida yoyote mwananchi anayoiona zaidi ya kuimbiwa nyimbo mpya na wanasiasa kila siku,hali ya uchumi inazidi kuwa mbovu,huduma za kijamii zinazidi kudorora lakini pale pale viongozi wanazidi kuingia mikataba mibovu na magabacholi kisha baadae mikataba hiyo inaishia kwenda kulipa faini hao magabacholi zaidi ya mara 10 ya mtaji wao!
hao viongozi usidhani ni mambumbumbu wanapoingia hiyo mikataba ala,wanajua kila kinachoendelea,wanajua madhara wanajua kila kitu ila kwani wao wanajali nini wakati wanataka kununua VX new model,kupeleka watoto wao ngambo wakasome,kumalizia kujenga ma-villa yao ili wayapangishe.
hata mkataba ukiwa mbovu vipi yeye anasign haraka haraka ili apate chake.
hakuna anayekemea uozo huu,hali inazidi kuwa mbaya kila siku wao hawajali maana wakiona mnapiga sana kelele wanajivua GAMBA.
hawajui(wanajua) kwamba tatizo haliko kwenye gamba peke yake lakini wanajali??
wananchi ilichobaki ni kuendelea kuhesabu tu miaka 50 ya uhuru hewalaa,miaka 47 ya muungano sawaaaa,miaka 100......... ok
siku zinaenda na hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

mkilalamika tena nambari wani wanajivua gamba lingine muziki unaendelea

No comments:

Post a Comment