Tuesday, 20 March 2012

Wakimbizi wauawa Somalia

 

 
Wakimbizi nchini Somalia
Wakimbizi sita wa kisomali wameuwawa katika shambulio la kombora mjini Mogadishu Somalia.
Vifo vilitokea baada ya makombora kuangukia kambi moja ya wakimbizi karibu na ikulu ya rais mjini Mogadishu.
Taarifa kuhusu shambulio hilo zinaendelea kujitokeza huku ikisemekana kuwa watu watano walijeruhiwa kwenye shambulio hilo.
Haijulikani aliyefanya shambulio hilo lakini wiki jana kundi la wapinaji wa Al Shabaab walifanya shambulio la kujitoa mhanga karibu na ikulu ya rais.
Al-Shabab linadhibiti maeneo mengi ya kusini mwa Somalia ingawa linaendelea kupoteza udhibiti huo.
Kundi hilo lililo na uhusiano na Al-Qaeda, lilishambuliwa na majeshi ya Ethiopia kutoka maeneo ya magharibi, huku jeshi la Kenya nalo likiwavamia kutoka kusini na hivyo likalazimika kuondoka mjini Mogadishu mwaka jana.

bbcswahili

No comments:

Post a Comment