Wednesday, 25 July 2012

SHEREHE ZA MASHUJAA ZAFANA DAR

Maofisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama wakimsuburi Rais Kikwete nje ya geti la kuingilia ili kuagana naye.
Gari la Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt, Shein ‘hayupo pichani’ likiwa tayari kumchukua kiongozi huyo baada ya sherehe hizo kumalizika.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange  na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema wakiwa  mstari wa mbele kuagana na viongozi mbalimbali waliohudhuiria sherehe hizo.
Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiagana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama  baada ya sherehe hizo kumalizika.
Mmoja wa askari wa enzi za kikoloni ambaye hakufahamika jina lake, akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na umuhimu wa siku ya mashujaa.
Hawa ni wakuu wawili wa vyombo viwili tofauti na muhimu vya ulinzi na usalama JWTZ na POLISI ambao ni Jenerali Mwamunyange na Inspekta Jenerali Said Mwema wakiwa wamesimama kikakamavu uwanjani hapo.
  Hawa ni maofisa wenye vyeo vya meja Jenerali ambao hawakufahamika majina yao, lakini mmoja ni kutoka Division ya vikosi vya anga  na mwingine kutoka Division ya vikosi vya nchi kavu wametambuliwa kutokana na mavazi yao, walinaswa na kamera yetu wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kama mwenyeji wao katika sherehe hizo. 
Askari wa zamani waliopigana vita enzi za ukoloni wakiwa katika picha ya pamoja baada ya sherehe hizo kufikia tamati.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za mashujaa zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Mohamed Shein na baadhi ya maofisa kutoka  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kama ilivyoada, Rais Kikwete alifanya shughuli zote zinazostahili ikiwa ni pamoja kusimika kisu, jembe na ngao kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa wetu.
Pia askari wa zamani waolipigana vita kuu ya pili ya dunia ambao wako hai, walihudhuria sherehe hizo.
 
(Picha/Habari na GPL)

No comments:

Post a Comment