Wednesday 9 February 2011

KIWANGO CHA ELIMU CHINI TANZANIA

Mwalimu na wanafunzi
hela ya kujenga shule hamna

serikali haina hela ya madawati


hakuna fungu la kununua madawati


wanaomba msaada

wakipewa wananunulia kau safiri ka wabunge na mawaziri

ISOME HIYO HABARI HAPA

inasikitisha sana kuona zama kama hizi za sayansi na teke linalokuja kama alivyosema bw mkapa,watoto wanaaga wanaenda shule halafu wanaishia kusoma katika mazingira kama hayo kwenye picha unategemea nini??
inatia aibu kuona viongozi wanakazana kudai waongezewe posho,wajengewe majumba ya ghorofa yenye swiming pull(sio poolwanunuliwe magari kama toyota vx V8 eti ndio linahimili mwendo mkali  kuwawahisha bungeni na mikutanoni wakasinzie(maana wamekesha nyumba ndogo na kwenye ulabu) na kesho kuna vikao.wanadai hii vx inakwenda mwendo kasi kwa hiyo litawafanya wawahi huko vikaoni(kama si kuwahi posho tena).

mafuta na service inalipa serekali na gharama yake unanunua vx lingine

mtoto hapo katoka nyumbani kapewa uji wa chumvi na andazi (kama mzazi wake mshua)
halafu anaelekea shule kitabu kitapanda kweli?
pia tusisahau ameagizwa aende na jembe na kidumu cha maji lita tano(maji yenyewe hayatoki kuna mgao mpaka uende kisimani) ili  kipindi cha kupumzika waende wakalimie bustani ya mchicha ya  mwalimu mmoja mnoko(ambaye fimbo zake hazivumiliki akikuchapa usipoenda na hivyo vitu).

hiyo bado mchana anarudi homu lunch anakutana na ugali na mlenda chuku chuku,jioni mtoto kamaliza masomo akirudi tena nyumbani nako anapewa karanga au machungwa na mzazi akatembeze.
embu nambie katika mazingira hayo ni kipi utakachofundishwa na kikakuingia akilini?ndio maana kiwango cha elimu kinashuka kila siku na hali ya maisha kuzidi kuwa mbaya. na kadri kiwango cha elimu kinavyoshuka na maisha kuzidi kuwa magumu ndio spidi ya matumbo ya viongozi wetu kuongezeka ukubwa inazidi,maana wanachopunjwa wananchi ndio wanaongezewa wao,wanachopokonywa wananchi ndicho wao wanachokiiba,wanachonyonywa wananchi ndicho wao wanachokihitaji ili waendelee kututawala wao na watoto wao na wajukuu na vitukuu na wajomba zao mashangazi na ukoo mzima.
iko siku haki na uhuru wa ukweli utarudi kwa mwananchi wa kawaida na ndipo nao watajua maharage ni mboga ya kula jela au ya kula sikukuu.
alamsiki

2 comments:

  1. Way to go ma brother!! Tunaitaji watanzania wengi wakereketwa kama wewe, wanaotumaia blog zao si kwa burudani tu bali pia kuandika vitu muhimu ktk jamii kama ivi. Next subject I suggest Dowans!! Tumechoka na hawa mafisadi jamani we need our own revolution....angalia Cairo!!//Mama E

    ReplyDelete
  2. its so sad kwamba viongozi wala hawashtuki na yanayotokea,wamekalia porojo tu za siasa utekelezaji zero.kenya hapo na rwanda wanatuacha vibaya sana

    ReplyDelete