Katika
siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi
ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye
vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo
yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi.
Kati
ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru
baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wiki
limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni
habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.
Idara inataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni za UZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali
ili
kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumiagazeti hilo. Idara
haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma
hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.
Matukio
yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho
ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia
upotoshaji huo uendelee.
Aidha,
tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa
dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo
kutuimarisha katika azma yetu ya kuhakikisha nchi yetu
inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine
vya Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.
No comments:
Post a Comment