Friday 27 July 2012

LONDON 2012 SHEREHE ZA UZINDUZI ZANUKIA



Mwenge wa Olimpiki, London 2012
Baada ya tetesi kuzuka kuhusiana na maandalizi ya michezo hiyo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema michezo ya mwaka huu itathibitisha kuwa Uingereza ina uwezo wa kufanya maandalizi kabambe.
Lenye Ijumaa ndiyo siku ya ufunguzi rasmi wa mashindano yatakayopeperushwa moja kwa moja kote duniani.

Bwana Cameron ametetea maandalizi ya mashindano hayo baada ya mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani Mitt Romney kusema kwenye mahojiano katika runinga ya NBC kwamba kuna matatizo katika usalama na tishio la mgomo wa maafisa katika maeneo ya mipakani.
Lakini baadaye bwana Romney alitabiri kuwa mashindano ya Olimpiki mjini London yatakuwa yenye mafanikio baada ya kukutana na waziri mkuu huko Downing Street.
Hapa Bw. Cameron aliukaribisha mwenge huo wakati uliposimama kwa muda ukiwa njia kuelekea Kasri la Buckingham.
Mwanamfalme William, mkewe na mwanamfalme Harry walikuwepo kuwakaribisha waliokuwa wakiiperusha mwenge huo kabla ya kupelekwa Hyde Park.
Meya wa mji wa London Boris Jonnson akizungumza mbele ya umati mkubwa wa watu 60,000 waliojitokeza kushuhudia sherehe hiyo aliwatakiwa kila la heri na kusema ''mashindano ya London yatakuwa ni ya kukata na shoka.''
Lakini pia alizungumzi mzozo uliokuwepo awali aliposema mbele ya umati huo: "kuna mtu anayeitwa Mitt Romney ambaye anataka kujua ikiwa tuko tayari. Tuko tayari? Ndiyo tuko Tayari!"

BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment