Friday 13 July 2012

Waasi wa Congo washambuliwa na UN.


Kiongozi wa M23 
kiongozi wa M23
Ndege za kivita za umoja wa mataifa, zimewafyatulia risasi waasi mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Afisa mmoja wa umoja wa mataifa amesema shambulio hilo dhidi ya waasi wa M23 limetokea kaskazini mwa Goma karibu na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda.
Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imeishutumu Rwanda kwa kusaidia waasi wa kundi la M23 hali inayovuruga amani katika eneo hilo.
Hata hivyo Rwanda imeendelea kukana kuhusika katika mgogoro wa Mashariki mwa Congo, ikisema mgogoro huo ni matatizo ya ndani ya Congo ambayo yameshindwa kutatuliwa.
Akizungumza katika kipindi cha mahojiano cha BBC, Hard Talk, Rais Paul Kagame wa Rwanda, amesema taifa lake halihusuki na matatizo ya Congo.
"hatuhusiki kwa vyovyote na vuguvugu la M23 hatuwasaidii wala kuwafadhili na wala hatuna nia ya kufanya hivyo kwa sababu hatujui wanapigania nini wala wanatetea nini.Kile tunachojua, uhusiano wetu na Congo ulikuwa mzuri sana kabala ya haya kutokea" Alisema Kagame.
Waandishi wa habari wanasema sio jambo la kawaida kwa kikosi hicho cha umoja wa mataifa kufanya mashambulio.
Wiki iliyopita waasi hao walivamia kituo kimoja cha Umoja wa Mataifa na kumuua mwanajeshi mmoja.
Rwanda, congo na mataifa mengine yameafikiana kuunda jeshi la pamoja kujibu mashambulizi hayo mashariki mwa congo.

bbcswahili

No comments:

Post a Comment