Hamisi Kiiza aliyepiga matatu |
MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Yanga leo wamefufua matumaini ya kutetea taji lao, baada ya kuitandika Waw Salaam ya Sudan Kusini mabao 7-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi C.
Nyota wa mchezo wa leo, alikuwa ni Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyeifungia timu yake mabao matatu na kuondoka na mpira.
Kiiza anayeingia msimu wa pili Yanga, alitikisa nyavu katika dakika za 19, 27 na 30, wakati Said Bahanuzi alifunga dakika za 15 na 17, Stefano Mwasyika dakika ya 25 na mwisho Nizar Khalfan dakika ya 75.
Klabu ya Sudan Kusini, taifa linaloshiriki kwa mara ya kwanza michuano hii, ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 88, mfungaji Hamisi Bashama. Katika mchezo wa kundi hilo, C uliotangulia, Atleltico ya Burndi ilitoka sare ya bila kufungana na APR ya Rwanda.
APR na Atletico zimejihakikishia kuingia Roo Fainali, wakati Yanga unaweza kusema kwa asilimia 90 imeshafuzu nayo, kwani ili isivuke, Waw Salam wanatakiwa kuifunga Atletico zaidi ya mabao 7-0.
MSIMAMO WA KUNDI C:
P W D L Gf Ga GD Pts
APR 2 1 1 - 7 - 7 4
Atletico 2 1 1 - 2 - 2 4
Yanga 2 1 - 1 7 3 4 3
Waw 2 - - 2 14 1 -13 -
SOURCE: http/bongostaz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment