Na Hamida Hassan
MATENDO anayofanya mwanamitindo Jackline Patrick wakati mumewe Abdullatif Fundikira akiteseka gerezani, yametajwa kuwa ni usaliti wa asilimia miamoja na kwamba kama hatajirekebisha, mwisho wake utakuwa mbaya.
Jack akiwa beach na Martin Kadinda.
Hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni kupatikana kwa picha
zinazomuonesha mwanadada huyo akiwa kimahaba zaidi na modo mwenzake wa
kiume, Martin Kadinda.Picha hizo zinawaonesha wawili hao wakiwa wamekumbatiana na kufanyiana mambo yasiyostahili kufanyika mbele za watu pale walipokuwa wakiogelea kwenye moja ya fukwe zilizopo jijini Dar na nyingine wakijiachia klabu.
Jack akiwa kwenye pozi.
Wakizizungumzia picha hizo, baadhi ya wadau walioziona walisema kuwa,
anachokifanya Jack si kizuri kwani ni usaliti wa dhahiri usiomfurahisha
Mungu.“Yule amefunga ndoa ya kifahari na Abdullatif, lakini leo hii mwenzake anateseka gerezani yeye anamsaliti huku uraiani, hii ni mbaya sana,” alisema Salim wa Mwananyamala jijini Dar.
Martin na Jack wakijiachia klabu.
Naye mama Oscar wa Kinondoni alihoji: “Huyu msichana anakosea sana
kufanya haya tena hadharani. Hivi yule mume wake anayeteseka kule
gerezani amemkosea nini mpaka anamfanyia usaliti wa wazi hivi?”
Jack akiwa klabu.
Mume wa Jack, Abdullatif Fundikira anayesota gerezani.
GPL
No comments:
Post a Comment