Monday, 27 June 2011
BOBAN AKABIDHIWA JEZI NO 3 MSIMBAZI
Na John Joseph
BAADA ya kurejea Msimbazi, kiungo Haruna Moshi ‘Boban’, (pichani) amekabidhiwa jezi namba 8 iliyokuwa ikivaliwa na nahodha wa Simba, Nico Nyagawa.
Tayari Kocha Mkuu wa Simba, Moses Basena, raia wa Uganda ameutaka uongozi kumuacha Nyagawa ili kutoa nafasi kwa vijana.
Boban ambaye amekuwa akivaa jezi namba 3 akiwa Simba na hata timu ya taifa, Taifa Stars, alianza kuonekana na jezi hiyo katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Vital ‘O ya Burundi juzi.
Kiungo huyo kabla ya kwenda Gefle IF ya Sweden, aliitumia kwa muda mrefu namba 3, hali iliyofanya iwe kama nembo yake.
Kukabidhiwa jezi hiyo kwa Boban, kumethibitisha kuwa tayari Nyagawa hatakuwa katika kikosi cha Simba msimu ujao kama lilivyoandika kwa mara ya kwanza gazeti hili, Ijumaa iliyopita.
Pamoja na Boban, mkongwe mwingine, Ulimboka Mwakingwe alishindwa kuirejesha jezi yake namba 14 baada ya kutua Msimbazi kwa mara nyingine.
Mwakingwe amekabidhiwa jezi namba 6 aliyoanza kuitumia juzi badala ya 14 ambayo kwa sasa inatumiwa na Shija Mkina aliyekabidhiwa wakati mkongwe huyo alipoachwa kwenye kikosi hicho kabla ya kusajiliwa na Majimaji ya Songea.
CHANZO:GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment