Tuesday, 28 June 2011

MSAADA WA MAFUTA YA KULA KWA SERIKALI YA TANZANIA!!


Balozi wa Japani nchini Hiroshi Kanagawa, akimakabidhi msaada wa mafuta ya kupikia katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdul Wakil, leo asubuhi Bandarini Dar es Salaam. Msaada huo wa mafuta ya kupikia umetolea na serikali ya Japani kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi waliopo katika kambi mbali mbali nchini


haya tena,ukishakuwa matonya huwezi kuwa na masharti ya msaada utakaopewa,huku ndiko tunakoelekea.kwanza najiuliza perezidaa amesafiri nini??maana angekuwepo huu msaada tungeona yeye anapokea.eeh ndio manaake,si juzi tu hapo tulipewa msaada wa yebo-yebo na hawa hawa wachina sijui wajapan.na muhishimiwa alikua pale kupokea.

haya sasa tunapewa mafuta ya kupikia!ingawa wanazuga yanaenda kwa wakimbizi lakini ni serikali ya tanzania ndio (maybe imeomba)imepewa msaada lmao!
kama msaada ni wa wakimbizi kuna viongozi wa WHO na UNHCR wanahusika na hii misaada.

huamini shauri yako,baada ya kupumzika kidogo na kituko cha bajaj ambulance na fire brigade bajaj sasa tumeenda kuomba mafuta ya kula.
na kiongozi mkubwa tu wa chama na serikali na wizara nyeti anachoma mafuta ya shangingi lake vx v8 kukimbia kumuwahi huyu mjapani anayeleta mafuta ya kupikia,lazima awahi maana akichelewa ataonekana ana dharau misaada na usikute hawa wajepu wameweka ntego tu,

maana huu utani mi nahisi kama vile mkulu yuko huko huko kwao hiroshima anapiga mizinga.sasa na wao kuthibitisha wameona watume mafuta ya kula ili waone kama tunahitaji msaada kweli ama vp,na huyu jamaa nahisi kahimizwa kuwahi msaada huo na labda kapigwa mkwara ole wake asionekane huko maana ataharibu dili.

haya umatonya unaendelea sasa baada ya mafuta ya kula,yeboyebo,vyandarua,tende na halua,nini kitafuata?muda si mrefu tutasikia ndege ya rais inachoma mafuta mpaka jamaika kuomba msaada wa pili-pili.kisha itaenda tena uchina kufuata koroboi na utambi,mara tutasikia imeenda tena kufuata msaada wa viberiti mara matango mara maembe.tujiandae tu.kuna muda wa miaka minne wa kuendeleea kufwatilia hili movie.baada ya miaka minne watachange stering lakini movie linaendelea
inaelekea hili movie refu kweli,sijui litaisha lini.

kazi kwenu wadanganyika

No comments:

Post a Comment