Wednesday, 17 August 2011

Barabara ya vumbi tosha Serengeti

Mipango iliyojaa utata ya kujenga barabara ya lami katikati ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na sasa baada ya ubishi na kuonywa kuwa mpango huo utaathiri mazingira na nyenzo za wanyama pori.
 
Thamani ya mazingira ni kubwa

Serikali ya Tanzania ilipanga barabara mbili yaani ya kutoka na inayoelekea kupitia mbuga hiyo kutoka ukingo wa Ziwa Victoria na pwani.
Lakini utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa mpango huo utaathiri vikali hali ya wanyama kama vile nyumbu na punda milia, ambao misafara yao ya kuhama, jambo ambalo linaangaliwa kama maajabu ya maumbile Duniani.
Serikali sasa imethibitisha kuwa barabara hiyo haitoguswa na itabaki kuwa ya vumbi.
Katika barua kwa Kituo kinachoshughulikia Hifadhi ya Mazingira Duniani mjini Paris, Idara ya mali asili na Utalii nchini Tanzania imesema kuwa sehemu ya barabara hiyo yenye umbali wa kilomita 50 itaendelea kusimamiwa kwa ajili tu ya utalii na utawala.
Serikali kwa sasa inatathmini njia nyingine ingawa itakuwa ndefu kuweza kuwafikishia wananchi wake huduma kupitia kusini mwa mbuga hiyo ya wanyama.
Barabara hiyo itaepuka maeneo yenye thamani ya kuhifadhi mazingira na athari zinazoweza kufuata.
Nyumbu wa Serengeti
Serengeti

Mwaka jana, kundi la wataalamu walionya kua barabara iliyopendekezwa kupitia mbuga ya wanyama inaweza kupunguza idadi ya Nyumbu wanaokadiriwa kuwa milioni 1.3 kufikia 300,000.
Athari kwa wanyama pori, wataalamu hao walionya kuwa Uchumi utaathirika mno kutokana na kupungua kwa wanyama hao.
Wataalamu hao waliitaja mbuga ya wanyama ya Serengeti kama mfano wa kipekee wa hifadhi ya wanyama wanaohamahama.
Safari ya kuhama hama kwa wanyama hao kila mwaka hushiriki takriban wanyama milioni 1.5, wakiwemo nyumbu na punda milia.
Wakati wanyama hao wakisafiri, huacha vinyesi ardhini, ambavyo husaidia kurutubisha mimea, huku nyayo zao zikizuwia ukuaji wa kupindukia wa nyasi.
Mabadiliko ya aina yoyote katika hali kama hiyo, wataalamu hao wamesema kwenye ripoti yao kwa serikali ya Tanzania, yatasababisha kupungua kwa wanyama wanaotegemea nyumbu na punda milia kama chakula chao kama simba,chui na duma.
Simba watatoweka
Simba

Hawa ni baadhi ya wanyama wanaovutia mno watalii.
Halikdhalika wataalamu hao wameonya kuwa barabara hiyo ingeweza kusababisha kubadilika kwa mimea na vilevile kusafirisha aina mbalimbali za magonjwa yasiyokuemo ndani ya mbuga.

chanzo:bbcswahili

No comments:

Post a Comment