Monday, 13 February 2012

U-TURN BLOG PAMOJA NA WADAU WAKE WATOA MISAADA KWA YATIMA

Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wakifurahia pamoja na watoto yatima walipofika katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini jijini Dar es Salaam,msaada wa vyakula na vitu mbalimbali uliokuwa na thamani ya shilingi Milioni 10 ulitolewa na U-turn blog kwa ushirikiano wapamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa amebeba mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es salaam.Wakati wa blog ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo vyenye jumla ya thamani ya shilingi Milioni 10.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wakifurahia pamoja na watoto yatima walipofika katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini jijini Dar es Salaam,msaada wa vyakula na vitu mbalimbali uliokuwa na thamani ya shilingi Milioni 10 ulitolewa na U-turn blog kwa ushirikiano wapamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi akizungumza na Watoto hao
Watoto wakikata keki
Sehemu ya Msaada uliotolewa kwa watoto hao
Watoto wakicheza.
Mmoja wa wasanii wanaochipukia Dogo Aslay akiwapagawaisha watoto wa naolelewa katika kituo cha Yatima cha Kurasini cha jijini Dar es Salaam,kwa wimbo wa naenda kusema kwa mama, wakati wa hafla ya Blogs ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda katika kituo hicho kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
Mkurugenzi. Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam,Msaada huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 10 ulitolewa kwa pamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu (NIMR) DK. Mwele Malecela akiwahudumia chakula watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Taifa cha Kurasini wakati wa hafla iliyoandaliwa na Blogs ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu, waliotoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na ngua vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
 
picha na habari na matukiomichuzi

No comments:

Post a Comment