Friday, 24 February 2012

WAVUVI HARAMU WA KICHINA WALIOKAMATWA NA MAGUFURI KWENDA JELA MIAKA 20


 Washitakiwa, Nahodha Hsu Chin Tai (kushoto) na Zhao Hin Guing waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania bila kuwa na kibali, wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 au kulipa faini ya Sh bilioni 21.Picha na Mohamed Mambo
---
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh bilioni 21 raia wawili wa China waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ) na kuwaachia huru wengine watatu.

Aidha, samaki waliokutwa kwenye meli hiyo hawatahusika na amri yoyote ya Mahakama hiyo kwa sababu Serikali ilishawagawa bure katika taasisi mbali mbali.

Pamoja na adhabu hiyo, Mahakama pia iliamuru meli ya Tawaliq I ambayo ilitumika kwa uvuvi huo haramu itaifishwe na Serikali ya Tanzania, kwa sababu ilikuwa ikifanya shughuli hiyo ya uvuvi kwa majina mbalimbali.

No comments:

Post a Comment