Friday, 13 April 2012

WABONGO NA KUTOKUWA NA UHAKIKA NA BIRTHDAY ZAO



imekuwa kawaida sasa kwamba inatokea mtu asijue umri wa mwanae mwenyewe wa kumzaa,ukimuuliza atakwambia nijue ili iweje wakati kuna mambo ya maana ya kufatilia?jamani umri wa mwanao hauna maana kufatilia?

nashindwa kuelewa hii inasababishwa na nini maana mimi mwenyewe niko kwenye mkumbo huo.

sasa hivi kuna hili sakati la mwigizaji wa kike anayekabiliwa na kesi ngumu ya mauaji LULU.kipindi cha nyuma yeye mwenyewe LULU alishawahi kujitangaza kafikisha miaka 18 na kufanya pati kubwa ya kuuaga utoto!kinachoshangaza ni kwamba baada ya kukumbwa na kesi hiyo imetokea watu waliokwenda kumwona na kudai kwamba wamethibitisha(kwa kuona cheti cha kuzaliwa) kwamba lulu hajafikisha miaka 18 bali ana miaka 17!
bado hatujapumzika na madai hayo baba yake akaibuka na kusema tena sio 17 ni 16 kabisaa mweeh!sasa tuamini lipi?

anyway tuachane na hayo,inabidi wandugu watanzania sasa tubadilike,hii mambo ya kutojua umri wa mwanao,au mama yako au hata wewe mwenyewe yashapitwa na wakati,sometime tutachekwa(kama hatujachekwa bado)maana sasa swala hili lishaota sugu
mi mwenyewe mmojawapo sina uhakika na umri wangu,nakumbuka huwa nasherehekea mara mbili tofauti(eeh ndo nilivyoambiwa,baba alitaja vingine mama vingine)!.
nilianza kusahau pia umri wa kijana wangu wa kwanza bryton nikashtuka sasa hivi nakumbuka kila kitu hata ukiniuliza usingizini nitataja,kwa huyu kijana wangu mwingine milton siwezi kusahau maana hiyo wiki kabla mamake hajajifungua sikulala na baada ya kuzaliwa pia sikulala wiki mbili mfululizo iweje nisahau?lazima nikumbuke,utasahau vipi wakati pia mama mtu miezi miwili kabla ya birthday ya mwanae lazima muandae zawadi na mipango kwamba siku hiyo mtafanyaje ama mtaenda wapi!
na hicho ndicho kinawafanya wenzetu wasijisahau siku ya kuzaliwa kwao.kwa mbongo sasa, utakuta siku yake ya kuzaliwa au kuzaliwa mwanae yeeh ndio kwaaanza yuko zake bar anagida ndovu na nyamachoma na kuangalia mechi ya manchester na asernal!akirudi home kama akiwahi yuko top akiambiwa chochote anasema niache nilale bana nimechoka,asubuhi tena anawahi job na hang-over yake,akitoka job tena programe continued yuko bar na kuangalia mechi tena ya liverpool!
mpaka siku anakuja kupata habari kwamba mwanae alizaliwa mwezi huo zishapita kama siku 10 zaidi kama si mwezi kabisa,na jamaa baada ya kuambiwa ataishia kusema"ayaaaaah nilisahau" ndio imetoka hiyo atasema tutasherehekea mwaka ujao,mwaka ujao ni yale yale mpaka miaka 7-10 inapita sasa mtu huyo atakumbuka kweli siku ya kuzaliwa mwanae??

inabidi tubadilike jamani nikianza mi mwenyewe(nshabadilika)na wadau mnaonisoma hapa tujaribu kufatilia hiyo kitu tutajisikia amani na raha moyoni kuwapa muda watoto+wenzetu nao siku yao wafurahi.

No comments:

Post a Comment