Wakazi
wa Jangwani jana tarehe 8 /jan/2012 waliitisha kikao katika eneo la
jangwani kujadili mustakabali wao baada ya kuwepo na mpango wa serikali
wa kuwataka wahame eneo hilo hatari wakati wa mvua.Diwani wa kata ya
Michikichini Gharib Diyami CCM lilipo eneo hilo ndiye alikuwa akiongoza
kikao hicho ambacho kilitawaliwa na jazba na hasira kali kutoka kwa
wananchi wote wakipaza sauti kulaumu azma ya serikali.Walimshambulia
diwani na kutaka kumuondoa madarakani kwa kile walichodai ni nguvu ya
umma.
Diwani huyo akionyesha hasira vilevile aliwaambia hawawezi kumfanya
kitu jambo lililoibua tafranikaribia na kuvuruga kabisa mkutano huo
MADAI YAO
Wakazi
wa jangwani wanadai wanao uzoefu wa ulaghai wa serikali kila
inapohamisha watu na kuwapeleka makazi mapya na kusema ikiwaonyesha
viwanja huwa inawatelekeza wasijue waanze vipi ujenzi na hata maisha kwa
ujumla.Hivyo hawataki kuhama mpaka wameridhika kuwa fedha wamepata za
kutosha.
Wanadai pia kuwa kuna namba zimewekwa katika baadhi ya nyumba na
nyingine hazikuwekewa hivyo kujenga hisia kwao kuwa fidia ya nyumba
itakuwa ya kibaguzi kwani hakuna anayejua namba hizo zina maana gani.
Wanadai hakuna haja ya kuhama mahali ambapo wamezoea na kwamba mafuriko
ni kwa sababu ya miundombinu mibovu,hivyo kushauri pesa zinazotaka
kutumika kuhamisha watu zitumike kujenga miundombinu bora eneo hilo
Wengine wanasema majengo yao ya jangwani yana gharama kuliko fidia
ambayo serikali huwa inatoa kwani wanaona kuna usiri kwenye swala la
kutathmini fidia hivyo wanahofia hasara kubwa na kukumbwa na umaskini
ikiwa watavunja nyumba zao
Wengine wanasema ni dhahiri serikali ndiyo inayowachanganya wananchi
kwani baadhi yao wamekuwa wakilipia kodi maeneo hayo na wanazo leseni za
ardhi na wengine wamemilikishwa kisheria na mahakama zaidi ya mara
mbili hivyo kuwaambia sasa wahame ni kuwaonea na kuwasababishia hasara
zaidi.
Kutokana na madai yote haya ni dhahiri wakazi wa jangwani hawataki
kuhama eneo hilo na wameazimia kuunda kamati ndogo ili kushughulikia
swala hilo haraka kwenye ngazi ya mkuu wa mkoa na hata waziri mkuu na
rais waliyedai walimchagua hivyo anapaswa kuwasikiliza.
Katika
hatua nyingine, mdau alipata shida kwani baadhi ya watu walionyesha
kukerwa na waandishi habari wanaokuja kuandika habari na kuwahoji watu
kisha habari zinatoka zikionyesha kawa wao ni wakaidi,wakanitaka
kuandika ukweli niliouona na ndicho mdau nilichofanya.Mwisho wananchi
wanasubiri kwa hamu ujio wa mkuu wa mkoa ili watoe dukuduku lao
KUTOKA MJENWABLOG
No comments:
Post a Comment