Wateja
wa Vodacom M-PESA wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa
kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya
mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-PESA.
Kuzinduliwa
kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-PESA
kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na
unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na
kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB..
Huduma
hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia
huduma yake ya M-PESA ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea
usumbufu wateja wa M-PESA wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu
kufuata tawi la Benki.
“Tunapoitambulisha
huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika
simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-PESA.Mteja wa M-PESA kuweza
kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za
mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa
Vodacom”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza.
Huduma
ya Vodacom M-PESA ya kwanza sokoni kutoka Vodacom mtandando unaoongoza
nchini ni kielelezo makini cha ubunifu na namna ambavyo Vodacom
imedhamiria kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya simu za
mkononi.
Ikiwa
na mawakala zaidi 20,000 nchi nzima M-PESA inabakia kuwa huduma salama
zaidi, ya haraka, uhakika na yenye kuaminika kwa ajli ya kuweka na
kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma na manunuzi mbalimbali, kulipia
kodi, kuchangia pensheni pamoja na kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya
sabini na tano ulimwenguni.
“Hakuna
mteja wa Vodacom M-pesa atakaesimama kwenye foleni au kulazimika
kutembea umbali mrefu kufuata tawi la benki yake ya CRDB, sasa wataweka
na kutoa fedha wakati wowte na mahali popote bila kuathiri shughuli
nyengine za kijamii na kimaendeleo ni wazi maisha yamekuwa rahisi
zaidi.”Aliongeza Bw. Rene
Tangu
ilipoanzishwa mwaka 2007, huduma ya Vodacom M-PESA imeendelea
kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa huduma yenye usalam zaidi,
yenye mtandao mpana wa mawakala mijini na vijijini na hivyo kuchangia
maendeleo ya jamii na biashara nchini kwa kuinua vipato vya wananachi
kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Kuweka fedha katika akaunti ya CRDB kutoka akaunti ya M-PESA,hatua ni kama ifuatavyo
- Piga *150#
- Chagua kulipia bili
- Ingiza namabri ya biashara ambayo ni 900500
- Ingiza nambari ya kumbukumbu ambayo ni namabri ya akaunti ya benki.
- Weka kiasi cha fedha mteja anachotaka kutoa katika akaunti ya M-PESA kwenda akaunti ya benki
- Ingiza nambari ya siri.
- Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha muamala.
Baada
ya hatua hizi mteja atapokea mara moja ujumbe mfupi wa maneno – SMS
kutoka M-PESA kuthibitisha muamala na baada ya dakika 8 atapokea ujumbe
kutoka benki ya CRDB.
Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya CRDB kwenda M-PESA hatua ni kama ifuatavyo
- Piga *150*03#
- Ingzia nambari ya siri
- Chagua nambari 3 (Hamisha fedha)
- Chagua nambari 3 (M-PESA)
- Chagua nambari ya akaunti yako ya Benki
- Thibitisha nambari yako ya simu
- Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuhamisha
- Thibitisha au batilisha. Na baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA na pia Benki ya CRDB unaothibitisha zoezi hili.
- Ili kuwa na uwezo wa kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda M-PESA ni LAZIMA kwanza mteja wa M-PESA ajisajili CRDB.
No comments:
Post a Comment