MR-ISAACKIN
ndugu wadau
ni mwaka na siku kadhaa sasa tangu nimeanza kublog hewani,mwanzo nilianza na social network ikiitwa vituuz.com lakini wapopo waliiingilia kati kisanii wakaanza kunisaidia ku-edit na kutuma maombi ya fwaranga kwa washabiki bila idhini yangu nikaifuta.ndipo nikaja na idea hii ya kuanzisha blogspot.ilikua kama utani lakini kwa ajili ya hobbie yangu ya uandishi siku nyingi iliwezekana.nashukuru mpaka sasa haijambo mwendo tunaokwenda nao unaridhisha kidogo ingawa si wa spidi kubwa.nashukuru kwa wadau wote walionitembelea na bado tuko kwenye ku-improve ili tuendelee kuwa na mashabiki zaidi na zaidi.blog yetu ina-base zaidi na mambo ya burudani kwa ujumla,urembo,muziki,movie,mpira chochote kinachohusu burudani utakipata hapa.politiki sio sana maana najua ni kuumizana vichwa tu,ingawa huwa nagusia gusia pale ninapoona vitimbi hasa vya wanasiasa wetu huko nyumbani.
mpaka hapo nimeishia mwisho na naahidi kuwa mtaendelea kupata vitu juu ya vitu na nakumbusha tena,mwenye maoni,malalamiko,ushauri wowote unakaribishwa ili tuendelee kuboresha blog yetu hii.na mwisho mwenye tukio,sherehe ama chochote anataka kiwe hewani asisite kunitumia e-mail(docmsaf@gmail.com)
adios
No comments:
Post a Comment