Monday, 17 January 2011
RAIS ANAPOTIMULIWA KWA MAWE
former Tunisia President Zine El Abidine Ben Ali's
after flee Tunisia president Ben Alli take refuge in this mansion Saudi Arabia.
habari za week-end waungwana
ijumaa tumeshuhudia kituko kingine kutokea bara la afrika,soo ilikuwa ni pale wanafunzi na raia walipoandamana nchini Tunisia kupinga rushwa ubadhilifu na hasa kitendo cha mwenzao kujiuwa mbele ya ikulu baada ya biashara yake ya mtaani kumwagwa na maaskari kisa hana leseni.baada ya hapo jamaa kaenda kujipiga kiberiti mbele ya ikulu ya nchi,na ndio hapo wanafunzi wenzie na raia wakaona haiwezekani jamaa yao kuonewa hivi hivi.wakaingia mtaani ilikuwa ni kupiga mawe kwa kwenda mbele,iwe askari trafiki mgambo ama yeyote anayehusiana na serikali alikuwa anakula mawe ya kufa mtu.movement yao ilipozidi kuelekea usawa wa ikulu prezidaa alipopewa taarifa akaona bora ajikate kungali mapema maana alijua jinsi kifo cha kupigwa mastone kinavyokuwa kichungu.usifanye mchezo bwana mtu kupigwa mawe mpaka kukata kauli cha moto unakiona.basi prezidaa kaingia mitini kuogopa mawe,lakini najiuliza pia ina maana jamaa hakuwa na njia nyingine yeyote ya kutuliza ghasia hizo?ama alikua siku nyingi kashaiba vya kutosha sasa anasubiria sababu tu ya kuanza,mkiangalia hilo jumba hapo alimowekwa usifanye mchezo bana,yaani inakua yeye kazi yake kula bata tu humo ndani na najua waarabu watakua wamemuandalia watoto wa kiarabu swaaafi humo ndani wanachoma udi tu na kumuimbia habibi habibi-halwa.haya bana tumuache aendelee kula raha.
ipate hiyo habari kiundani gonga HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hahahahaha ikibidi kama mbwai ni mbwai kama walivyosema wagosi waka.viongozi smtime wanasahau kama wao sie ndo tunawachagua.ili kupata amani,vita lazima. ndo hivyo!
ReplyDelete