Wednesday, 19 January 2011

WACHINA NA BONGO YETU

kwanza walitupa yebo-yebo na wakamuita rais mwenyewe akapokee

na basikeli sheng-zheng

na tuku-tuku zao zenye majina ya ajabuajabu kama better,jinyee,jide.

kisha majuzi hapa wakajenga shule pale kijijini kwa mtukufu msoga
na wakamuita mwenyewe mtukufu sana akaizindue
BAADA YA HAPO
KILICHOTOKEA




1.Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC) linalosimamia mradi huo, Dk. Clisant Mzindakaya, akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya China ya Sichuan Hondga, Liu Canglong, kabla ya kuanza mazungumzo ya maafikiano kuhusu kuanza kwa mradi wa Mawe wa Mchucghuma na wa Chuma wa Liganga,leo mjini Dar es Salaam.
-----
Akizungumza na waandishi wa Habari, leo kabla ya mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Gideon Nasari alisema, mazungumzo hayo yatachukua siku nne, na taarifa kuhusu hatma ya mazungumzo ya maafikiano hayo itatolewa baadaye.

Lakini akadokeza kwamba mradi wa makaa ya mawe unatarajiwa kuanza miezi sita baada ya maafikiano kufikiwa lakini zaidi ya hilo utakamilika kabla ya Rais wa awamu ya nne, Dk. jakaya Kikwete kumaliza muda.

usishangae ndiyo yanayotokea hayo huko nyumbani,nakumbuka story ya zamani ya mababu zetu kupewa gololi kisha wao kuwapa almasi wakoloni.sasa ndio haya yanatokea sasa hivi na utandawazi wote huu.hawa wanaojiita wawekezaji washagundua weakness za viongozi wetu basi nao wanazitumia ipasavyo.sasa wanasema wamekaa mazungumzo sijui makubaliano hamna kitu pale zaidi ya kukubaliana percent gani iende kumfuko kwao basi.na hao wachina wameambiwa kabisa wachote hicho chuma na makaa ya mawe  kujilipa kabla prezidaa hajamaliza muda. na hawa jamaa tusifanye nao mchezo maana wanafanya kazi kama sisimizi,tusishangae hiyo miaka mitano wakakomba hicho chuma mpaka ukoko.jamani nchi inaenda wapi sijui,tusipoangalia tutadaiwa na wanetu baadaye.

sasa naanza kuelewa pale dakta jk wa ukweli aliposema"ukitaka kula shurti uliwe kidogo"sasa hii imekuwa kinyume
"ukitaka kuliwa shurti ule kidogo"

No comments:

Post a Comment