Monday, 28 February 2011

Mwanafunzi Aliyefia Gesti Alikuwa ni Muathirika


Msichana huyo aliyetajwa kwa jina la Amina Ramadhani anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30 , alikutwa juzi usiku akiwa amekufa katika chumba cha nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Mkomboni Bar & Guest House, iliyopo Mtaa wa Mkunguni Kata ya Hananasifu jijini Dar es Salaam.

Msichana huyo alikutwa na Kitambulisho cha Ubungo High School, kinachomuonyesha kuwa amemaliza elimu ya Sekondari katika shule hiyo mwaka 1997, pia alikutwa na Cheti kinachomuonyesha kuwa ni muathirika wa Ugonjwa wa Ukimwi aliyekuwa akitumia dawa za kurefusha maisha.

Akizungumza na Nifahamishe.com mhudumu wa Gesti hiyo, Lydia Paul, alisema kuwa alimpokea msichana huyo juzi majira ya saa kumi jioni akiwa ameongozana na mwanaume na kufika eneo la baa na kuagiza soda.

“Baada ya muda msichana yule aliingia ndani na kutoa noti ya Sh. 10,000, ili apatiwe chumba, na baada ya kumaliza taratibu za kulipia na kuandika jina lake pekee alirudi nje na kumchukua mwanaume huyo na wakaingia chumba hicho namba sita pamoja", alisema Lydia.

Kwa kipindi hicho chote hatukuweza kusikia kelele hadi jioni walipotoka na kuingia bafuni kwa ajili ya kuoga na kurejea tena ndani. Ilipofika mida ya saa moja jioni, yule jamaa alitoka na kutuaga kuwa anakwenda kumnunulia chakula mwenzake.

"Alipoondoka nilikuwa nikitoka nje na ndipo nikaona mlango wa chumba hicho ukiwa wazi nikajaribu kumuita yule binti ili aurudishie mlango, lakini akawa kimya na nilipojaribu kugonga bado akawa kimya ndipo nikaingia ili kumuamsha nikijua amepitiwa na usingizi, lakini baada ya kuingia nikamkuta akiwa amejifunika gubi gubi na kanga huku mikono yake ikiwa nje"

"Kila nilipojaribu kumuamsha hakuweza kuitika, nikawaita wenzangu tukaanza kumpepea baada ya kumfunua na kumuona kuwa hatingishiki tukijua amezimia, na ndipo tukaamua kwenda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi cha Mkunguni hadi saa nne usiku askari walifika na kumpekuwa na kuchukuwa mwili huo” alisimulia Lydia.

Nao baadhi ya mashuhuda ambao hawakupenda kutaja majina yao, walisema kuwa siku tatu zilizopita katika gesti hiyo hiyo, walimuona mdada mmoja akitoka mbio ndani huku akipiga makelele.

“Siku kama tatu zilizopita tulimuona mwanadada akitoka mbio humo ndani huku akipiga kelele na akiwa na nguo zake mkononi, na majuzi pia tulipata stori kuwa jamaa huyo huyo aliyeingia na marehemu, aliingia na mdada mwingine lakini walipoondoka katika chumba chao zilikutwa damu zilizokuwa zimetapakaa” alisimuliwa mmoja wa mashuhuda.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufika eneo la tukio juzi usiku na kumkuta marehemu.

Aidha alisema kuwa baada ya kumpekuwa marehemu huyo walimkuta na kitambulisho cha Ubungo High School kinachoonyesha kuwa alianza kidato cha kwanza katika shule hiyo, 1996 na kumaliza 99, pamoja na cheti cha kuchukulia dawa za kurefusha maisha katika kituo cha Hospitali ya Sinza.

“Katika cheti hicho kilichokuwa na namba 002061, kilionyesha tarehe ya mwisho kuchukua dawa katika kituo hicho ilikuwa ni Januari 26 mwaka huu na alitakiwa kurudi kuchukuwa tena dawa hizo Februari 24 mwaka huu", alisema kamanda Kenyela.

Na pia alikutwa pembeni yake kukiwa na mipira miwili ya kiume na mmoja ukiwa umetumika” alisema Kenyela

Hata hivyo gesti hiyo inaonekana kugubikwa na wimbi la aina hiyo kwa kuwa tangu ilipoanzisha kutoa huduma mpaka sasa tayari wasichana watatu wameshafia ndani ya gesti hiyo.
KWA HABARI NA PICHA ZAIDI  GONGA HAPA

No comments:

Post a Comment