- HALI ya amani imepotea kabisa katika ndoa ya kiungo nyota wa Yanga, Shamte Ally baada ya kugundua mkewe ana uhusiano na mtu mwingine wa kimapenzi.
- Chanzo cha uhakika kimeeleza Shamte yuko kwenye mgogoro mkubwa na mkewe baada ya kunasa idadi kubwa ya ujumbe mfupi kwenye simu ya mkewe kutoka kwa Athumani Machuppa aliyewahi kung’ara kisoka akiwa na Simba.
- “Kuna mgogoro mkubwa sana kati ya Shamte na mkewe anayefanya kazi kwenye ubalozi wa nchi fulani hivi hapa jijini Dar es Salaam. Unajua imechukua muda mrefu hadi jamaa akagundua kuwa mkewe amekuwa akimsaliti,” kilieleza chanzo na kuendelea:
- “Mkewe alianza kutumia namba ya siri ambayo kila akifika nyumbani alikuwa anaitoa ile laini na kuendelea na ile ya kawaida. Shamte aliposhitukia akaiiba na kubaini kila kitu.”
- Baada ya hapo, gazeti hili lilimtafuta Shamte na katika mahojiano yaliyofanyika jana, kiungo huyo aliyerejea kwa kasi uwanjani baada ya kuwa majeruhi alitamka wazi kuwa Machuppa ndiye mbaya wake.
- “Nimefanya uchunguzi, hakuna ninachobahatisha, nimekamata meseji zake kwenye simu ya mke wangu, nimeumia sana,” alisema Shamte.
- Shamte alizionyesha meseji hizo kutoka kwa Machuppa kwenda kwa mkewe, baadhi zilieleza hivi: “Achana na mumeo tuoane baby…au hauko tayari, I wanna marry you.”
- Nyingine ikaeleza: “Baby want you…nakutamaniii jamani…tunajiandaa kwenda airport, tuko ndani ya basi…mi sitaki kurudi Sweden, nimekwambia nataka kucheza hapa.”
- “Nafikiri umeziona, kuna meseji zaidi ya 30 na nyingine mke wangu amemtaja jina kabisa. Nimejaribu kumpigia kwa simu ya mke wangu, alipojua ni mimi, mara moja akakata na hadi leo simu imezimwa,” alisema Shamte akionekana ni mwenye huzuni sana.
- Juhudi za kumpata Machuppa anayechezea Vasalunds IF ya Sweden ziligonga mwamba baada ya simu yake kuwa inaita tu bila ya kupokelewa.
- Championi lilimsaka mke wa Shamte ambaye alipopokea alisema: “Kweli ameziona hizo meseji, sasa si ahakikishe kwanza. Kwa sasa nipo kazini, naomba uniache.”
- Baada ya hapo alikata simu na hakupokea tena kila alipopigiwa, hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu.
toka GPL
hapoooo!
ReplyDelete