Monday, 7 November 2011

bei ya madafu ya leo leo hii


sijui tunaelekea wapi sasa maana ni kama vile zimbabwe hiyooo inakuja,sasa hivi ukitoka out na vi laki viwili vitatu ni hela ya kiingilio na maji ya kunywa tu yaani kurudi bila change ni kawaida kabisa.kwa mtaani uswazi ndiosio kama zamani,nyama juu,sukari bei juu,mafuta taa juu,samaki ndo usiseme hawashikiki,kuku ndio kabisaaaahiyo bei yake si mchezo.

sasa iliyobaki ni kupiga michicha na dagaa kwa kwenda mbere,lakini maisha poa mi najionea kwa hizo dagaa na mchicha nnatafuna kweli vile nilizi-miss yaani wenyeji hawanielewi kabisa maana wao kula hivyo vitu na maharage ni kama adhabu.

sasa kwa hali kama hii inakuaje?vyombo husika ni kama havipo na wala havioni kama kuna umuhimu wa kushughulikia huu mfumuko wa bei ya fedha zaa nje.kwa sasa imekua kawaida kabisa ukienda madukani na mashuleni wakakwambia ulipe kwa dola maana dafu letu halina thamani kabisaa

kwa hali kama hiyo mshahara wa mtu serikalini analipwa laki mbili hivi ataishije?ndo mana usiombe ufike huko hospitali,polisi au mahakamani utakoma kuringa,unaweza kutajiwa bei ya rushwa mfanyakazi anayotaka ili akuhudumie ukazimia kabisa.na hali hiyo inaeleweka kila mahali kiasi kwamba mwananchibidi wabargain na nesi au polisi au hakimu akupunguzie kiasi cha bei ya kumpa rushwa atoe huduma ni kawaida.
bandugu huko mliko zichangeni vya kutosha mrekebishe maisha hapa mwende sawa.tuambizane ukweli ni kwamba bongo kimenuka kwel kwel sasa.
ni kama jahazi limeachwa liende lenyewe bila nahodha
viongozi wako kwenye honeymoon,mpaka warudi jahazi lishazama.

na bado naskia lengo ni dollar1 kufikia kuuzwa tsh 2000 

1 comment:

  1. ebwana upo sahihi mkuu chamsingi ni kukaza tu ili twende sawa

    ReplyDelete