Friday, 16 December 2011

ALIYEKUWA RAIS WA UFARANSA JAQUE CHIRAQ AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA UFISADI


Mahakama nchini Ufaransa imemhukumu kifungo miaka miwili rais wa zamani Rais wa zamani wa Ufaransa, Jacques Chirac, kwa ubadhirifu wa fedha na kukosa uaminifu kwa umma.
Amepewa hukumu ya miaka miwili ambayo si lazima aitumikie gerezani.
Bwana Chirac amekutwa na hatia ya kutengeneza ajira hewa kwa wanachama wa chama chake cha Rally for the Republic (RPR) wakati alipokuwa meya wa Paris.
Rais huyo wa zamani aliyetumikia nafasi hiyo kwa miaka kumi na miwili mpaka mwaka 2007 ni kiongozi wa zamani wa kwanza wa nchi kuhukumiwa tangu Marshall Philippe Petain, kiongozi wa kivita wa zamani mwaka 1945 aliyeshirikiana na Manazi.
Bw Chirac mwenye umri wa miaka 79 hakuwepo mahakamani wakati wa kesi yake kwa sababu inaarifiwa kuwa anaumwa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu au kusahau lakini amekana kuhusika na makosa hayo.
Upande wa mwendesha mashtaka ulimtaka jaji kumfutia kesi hityo Bw Chirac na wengine tisa walioshitakiwa katika kesi hiyo. Wawili kati ya tisa walifutiwa mashtaka na wengine saba walikutwa na hatia.
Mwaka 2004, wakati wa urais, tawkimu kadhaa zikiwemo za Waziri wa sasa wa mambo ya nje Alain Juppe walihukumiwa kuhusika na kesi hiyo.
Bw Juppe alipewa kifungo cha miezi 14 nje
Mwandishi wa BBC mjini Paris anasema hukumu hiyo imekuja kama msshangao kwa umma wa Wafaransa kwa sababu upande wa mwendesha mashtaka ulisema kuwa haijathibitishwa kuwa Bw Chirac aliyajua matukio binafsi ya ajira hewa. Itaonekana kama doa katika tabia yake, anaongeza mwandishi wa BBC.

'Uvunjaji wa tabia njema'

Kesi hiyo iligawanywa katika sehemu mbili; kwanza kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma na kuvunja uaminifu kwa umma kutokana na ajira hewa 21: na pili mashtaka dhidi ya mgongano wa maslahi kuhusu ajira saba
Alikutwa na hatia katika makosa yote.
Rais huyo wa zamani ambaye alikuwa na kinga dhidi ya mashtaka wakati akiwa Rais alikuwa anakabiliwa na miaka kumi gerezani na faini ya euro 150,000 kwa ajira hewa ya zaidi ya maafisa 20.
"Jacques Chirac amevunja majukumu ya tabia njema inayotakiwa kwa maafisa wa umma kuharibu maslahi ya wakazi wa Paris" Jaji wa mahakama hiyo Dominique Pauthe alisema.
Ingawa mwenyewe hakuwepo mahakamani binti wa Bw Chirac Chirac alikuwepo kusikiliza hukumu hiyo.
Daktari wa rais huyo wa zamani amesema ana matatizo ya kupoteza kumbukumbu ambayo yanababisha kusahau. Timu yake ya sheria sasa inatathmini iwapo itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
"Kwa wale wanatarajia kesi kutupiliwa mbali au angalau kukosa adhabu uamuzi unaweza kuwa unaokatisha tamaa." Alisema mmoja wa mawakili wa Bw Chirac, Georges Kiejman.
"Naamini hukumu haitabadili kabisa upendo wa watu wa Ufaransa ambao bado wanao kwa Jaques Chirac."

1 comment:

  1. hahahahahahahahaha mbona bongo hakuna hukumu jamani?????maana kwa kesi hizo sijui atabaki nani maana hadi huyo hakimu pia itabidi ajihukumu na yeye mwenyewe!!!

    ReplyDelete