Monday, 5 December 2011

TWANGA KUREJEA NCHINI LEO



Twanga Pepeta ilipokuwa huko ilifanya maonesho matatu makubwa katika miji tofauti ya London. Milton Keynes na Birmingham. Onyesho la kwanza ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya ufunguzi wa sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika Nchini Uingereza ambalo lilihudhuriwa Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Peter Kallaghe, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na Kaimu Balozi Mhe. Kilumanga.

Twanga Pepeta ilifanya ziara Nchini Uingereza kufuatia mwaliko wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Uingereza na Jamii ya Watanzania waishio Nchini Uingereza chini ya Uratibu wa Urban Pulse na Miss Jestina Blog wakishirikiana na ASET.

Hii ni mara ya pili kwa Bendi ya Twanga Pepeta kuzuru Uingereza mara ya kwanza ilikuwa mnamo mwaka 2007. licha ya kuzuru Uingereza Twanga Pepeta ilishawahi kuzurru Nchi mabalimbali za Bara la Ulaya kama Uholanzi, Norway na Sweden kwa lengo ya ziara ya kimuziki.

Mara baada ya kurejea Nchini Twanga Pepeta inataraji kuungana na wenzao waliobaki kufanya maonyesho yao ya kila wiki kwa kuanzia Jumatano watakuwa Club Billicanas, Alhamis watakuwa Equator Grill Mtoni, Ijumaa watasherehekea miaka 50 ya Uhuru katika ukumbi wa Da West Park uliopo maeneo ya Tabata. Jumamosi watakuwa Mango Garden Kinondoni na Jumapili mchana wataanzia kutoa burudani katika Bonanza Leaders Club Kinondoni na baadae watakuwa Msasani Beach Club.

Twanga Pepeta iliondoka na wasanii 12 ambao ni Kiongozi Mkuu Luizer Mbutu, Kiongozi Msaidizi Saleh Kupaza, Charles Baba, Venance na Khamis Amigolas. Wengine ni Miraji shakashia, James Kibosho, Victor Nkambi na Jumanne Jojoo. Wengineo ni Asha Said “Sharapova”, Maria Soloma na Betty Johnson “Baby Tall”


Hassan Rehani
Meneja ASET.

No comments:

Post a Comment