Tuesday, 6 December 2011

mrembo wa kitanzania aliyeolewa na kibabu cha kiingereza anusurika kukatwa mikono

Tan Express on Victoria Road

Mfanyabiashara ambaye alimtishia kumkata mikono mkewe afungwa jela miezi 15 baada ya kuishi kwa muda wa miezi saba tu.

William Porter alikutwa na hatia ya kumdhuru mkewe kwa kutumia kisu cha jikoni. Mahakama ya York Crown Court ilimkuta na hatia hiyo ya kumshambulia mkewe mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni raia wa Tanzania.

Porter, anaeishi Belgrave Crescent ambaye anamiliki saluni ya Tan Express, alikanusha madai hayo ya kumdhuru mkewe Saada Mwiazimu. Ingawa alikuwa akishikilia kuwa hakuwa na hatia lakini alifungwa kwa muda wa miezi 15.

Sakata hilo la Saada kujeruhiwa kwa kisu lilitokea mwezi juni mwaka jana wakati Saada na mumewe walipokuwa kitandani wakiangalia DVD baada ya kurudi nyumbani kutoka katika mlo chakula.

Mahakama ilielezwa kuwa udhaifu wa mapenzi wa mume huo ndi ulikuwa chanzo cha mgogoro huo hivyo William alimdondosha chini Saada kwa kumpiga teke na baadae kumjeruhi kwa kisu mikononi.

Mahakama imeelezwa kuwa bado anaonekana kuwa na makovu.

Mwanzo wa yote ilikuwa mwaka 2009 wakati William aliposafiri kuja Tanzania kuonana na Saada ambaye alimjua kupitia dada yake ambaye yupo Uingereza na kuanza kuwasiliana naye kwa kutumia email.

Kukutana kwao kulipelekea kuanza kwa uhusiano wa mapenzi ambapo William alimualika Saada Uingereza ili pia aje akutane na dada yake. Ujio huo haukudumu muda mrefu kwani Saada alikamatwa akiishi Uingereza akiwa amepitiliza muda wake wa kuruhusiwa kuishi Uingereza. Alirudishwa Tanzania na maafisa wa uhamiaji wa Uingereza.

William aliamua kutumia njia ya kumuoa Saada ili waweze kuishi pamoja Uingereza. William kwa mara nyingine alikuja Tanzania na kumuoa Saada mwezi januari mwaka jana na kuanza mikakati ya kumtafutia viza ili aruhusiwe kuishi Uingereza. Baada ya vipingamizi vya hapa na pale hatimaye Saada alipewa viza na kuwasili Uingereza mwezi mei mwaka jana.

Saada aliishi pamoja na William kwenye nyumba ya juu katika ghorofa linalomilikiwa William ambapo mke wa zamani wa William alikuwa akiishi nyumba ya chini.

Hatimaye mwezi mmoja baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo ndipo sakata hilo lilipotokea na kupelekea Saada abaki na makovu kwenye mikono yake.

Akijitetea kabla ya kuhukumiwa kwenda jela miezi 15, William aliiambia mahakama kuwa kesi hii ilipangwa na mkewe ili aweze kumkimbia aendelee kuishi Uingereza.

No comments:

Post a Comment