Tuesday, 14 December 2010

MUUAJI WA MALMO YASEMEKANA CHIZI



isome habari hiyo HAPA

ukishangaa ya musa utayaona ya firauni,wakati bado watu wanaugulia maumivu ya kukoswakoswa na yule gaidi hapa stockholm jumamosi.nafikiri bado mnamkumbuka huyu jamaa hapo juu aliyetokea kuwa tishio huko malmo baada ya kuanza kuwa shoot watu hasa wahamiaji.akafanikiwa kuua wawili na kujeruhi watano kama sio saba.bahati nzuri waswede wakamkamata na hiyo ni baada ya watu kuppiga kelele sana maana mwanzo hawa jamaa waliendelea na usemi wao"i dnt care" watu walipokuwa wanakoswakoswa,yaliyotokea ni kwamba hii kesi bado inaendelea na sasa hawa watu washaanza ku sy-mpathise hii kesi iwe laini laini,tusishangae huyu bwana akaachiwa bila chaji yoyote.kinachosemekana ni kwamba wamehisi huyu bwana anasumbuliwa na uchizi"mwezi mchanga"wa muda hivyo bado wanafikiria kama wamempeleke hospitali ya vichaa ama jela!!.
hivi ni swala la kuulizana kweli kuhusu kesi ya mtu kuua??tena sio kuua mara moja mara mbili na kujaribu kuua mara tano zaidi,ni kweli utasema huyu mtu ni chizi??chizi anajua kubeba bastola ku-load risasi na kutoka nje kuwafatilia wahamiaji na kuwashuti,kwanini uchizi wake asijilenge yeye basi.ni vipi wale waliokufa je,watarudishiwa uhai wao eti kisa muuaji hakudhamiria ndio uchizi umefanya afanye hivyo?hapo ndio justice system ya sweden inapochosha.ama ni kwa sababu aliwalenga wahamiaji basi hawa watu wanadharau tu maana wanaona ni kama alikuwa analenga mbwa na si binadamu.hivi pata picha angekuwa mjamaa mmoja kutoka africa ndio anafanya haya mambo ya kulenga watu na kuua angechukuliwa hatua gani na hawa jamaa.hivyo ndo akili mukichwa tujue tupo hapa tufunge mikanda.sio kwetu hapa.

No comments:

Post a Comment