Thursday, 2 December 2010
WASANII BONGO WANAVYOLIZWA
Icon wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, mwishoni mwa wiki aligeuka kiroja baada ya kuangua kilio hadharani kufuatia kushuhudia muvi yake mpya ya Uncle JJ ikionyeshwa kwenye ‘vibanda umiza’ siku moja kabla ya uzinduzi wake.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, kisanga hicho kilitokea maeneo ya Yombo Dovyo Relini, wilayani Temeke jijini Dar wakati nyota huyo wa Filamu ya ‘More than Pain’ akiwa kwenye mishemishe zake.
Imedaiwa kwamba, akiwa eneo la Reline aliuona ubao wa matangazo nje ya kibanda kimoja cha kuonesha sinema ukisomeka kuwa saa nane mchana, kutakuwa na muvi mpya ya Uncle JJ, jambo lililomshangaza kwani alikuwa bado hajafanya uzinduzi wa filamu hiyo.
“Jamaa alikuwa kwenye pita pita zake, alipofika hapa akaliona hilo bango akaamua kupaki gari yake nakwenda kujua kilichoendelea ndani ya kibanda hicho, alipokuta watu wanaangalia muvi yake, alishikwa na uchungu na kuanza kulia,” kilisema chanzo chetu.
Umbeya zaidi kutoka kwa shuhuda huyo unasema kuwa, kufuatia Kanumba kuumizwa na kitendo hicho
alimbana mwenye kibanda amueleze alikoipata muvi yake.
Akiendelea zaidi shuhuda huyo, alishusha data kuwa Kanumba alimuamuru mmiliki wa ‘ofisi’ hiyo kuitoa Cd aliyokuwa akiionesha huku akitishia kumpa kichapo endapo angegoma jambo ambalo jamaa alilitekeleza na Kanumba akaondoka.
Paparazi wetu alipomuendea hewani Kanumba na kuhoji juu ya kizaazaa hicho, alikiri kutokea na kuongeza kuwa aliumia sana baada ya kuona watu wanaiingalia muvi ambayo hata uzinduzi wake ulikuwa haujafanyika.
“Niliumia sana mpaka nikafikia hatua hiyo kwa sababu nimetumia gharama kubwa kuiandaa muvi hiyo lakini wajanja wanakula kiulani,” alisema Kanumba. Hata hivyo, muvi hiyo tayari imeshafanyiwa uzinduzi wake na sasa inapatika sokoni katika vipimo vya DVD vhs na VCD.
CHANZO:G.P.L
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment