Tuesday, 21 December 2010

SAFARI YA MWISHO YA ABUU SEMHANDO"BABA DIANA"


juu ni pikipiki aliyopata nayo ajali na chini ni wakati anazikwa
ABUU SEMHANDO ENZI ZAKE

sijui ni kutokana na mshtuko ama vipi,nilishindwa kumuongelea huyu mkongwe wa muziki aliyetutoka ghafla hapo jumamosi usiku kwa ajali.nilimfahamu abuu miaka hiyo 96-97,pale tulipokuwa tukifanya kazi pamoja pale new silent club(najua wengine mtasema huyu nae anamjua kila mtu).kipindi hicho ndio bendi ya diamond sound"wana ikibinda nkoy" ndio ilikuwa imeanzishwa tu na ilikuwa inazinduliwa rasmi.katika watu pekee waliokuwemo kwenye bendi hiyo ambao ni watz ni huyu bwana pekee aliyepata nafasi(maana wanamuziki wengine wote walikuwa wacongo).abuu alikuwa mtu mmoja charming na anayeongea na kila mtu hakuwa na maringo ya namna yeyote(maana wale wacongo ilikua tabu kipindi hicho)na alikua anaongea na kila mtu.nakumbuka baada ya kuzindua pale hatukukaa sana maana mie niliacha kazi baada ya uzinduzi tu wa bendi,nilishtukia ubabaishaji nikaanza nikawaacha wengine.abuu alivumilia sana na hiyo bendi sio siri,maana baada ya uzinduzi kulitokea na ubabaishaji wa hali ya juu wa mmiliki wa club hiyo.baada ya kutoka hapo nadhani abuu alikuwa ni mmoja kati ya wanamuziki waliojiengua diamond kisha kuunda dar musika iliyosimamiwa na marehemu choggy sly.dar musika haikudumu na ndio huyu bwana kuangukia twanga pepeta aliyodumu nayo mpaka mauti yalipomkuta.tukija kwenye utaalamu wa kuzikaanga hizo wanaita chipsi au mihogo,abuu alikua ni mmoja wa wataalam wakuu kabisa kwenye nyanja hiyo.nilikuwa mshabiki wa twanga mkereketwa hivyo naelewa huyu bwana alivyotia mchango wake katika ukuzi wa bendi ile pamoja na kusimamia nidhamu.jamaa alikua akikaa kwenye kiti sie wakereketwa ndio tunanyanyuka maana tunajua mzee mzima kaingia sasa ni muda wa kulipepeta twanga sebene.alikua akishaingia mzee pale nyuma,halafu kwenye tumba kuna mcd(naye alitoka diamond nilimkaribisha twanga siku ya kwanza anatambulishwa aliyoacha diamond sound kuhamia twanga) ,kuna yahaya mkango kwenye bass,kuna jojo jumanne kwenye solo,pale mbele unoz ulikua unamkuta jessica charles na luiza mbutu enzi hizo wakisindikizwa na amigolas(mwanamuziki wa kwanza kupendwa twanga,kabla hawajaanza kutunga nyimbo zao walikua wanaimba copy na amigolas alikua anaimba copy zote za kizaire),kinanda unamkuta profeshenee kibode mkambi,kushoto kuna ali choki,kulia kuna banza stone mwana masanja.timu ilikua imekamilika.tafuta nyimbo kama laitness,kisa cha mpemba na kuolewa.utajua naongelea nini.kweli tulikua tunatwanga kina mama wanapepeta huku BAPA linafanya kazi yake kichwani.ni kweli kwamba muhimili wa bendi umeondoka lakini najua twanga haitatetereka kwani kuna huyu kijana james kibosho  (niliona kipindi cha nyuma akielekezwa kuzipiga drums inavyotakiwa na baba diana) ambaye amechukua ukanda nayeye ni mtaalam mkali tu sasa hasa kwa hizi nyimbo za kisasa anajua kuzichapa hizo drums inavyotakiwa.najua hakijaharibika kitu.

MUNGU AMLAZE ABUU SEMHANDO PEMA PEPONI AMINA.



No comments:

Post a Comment