Wednesday, 13 July 2011

KILIMANJARO FC IMECHAPA TIMU YA KENYA 8-1 KOMBE LA AFRICAN CHALLENGE HAPA STOCKHOLM


KIKOSI KAMILI KILICHOFANYA MAUAJI HAYO

WACHEZAJI WA KILI FC KATIKA HEKA HEKA

sijui kama mchango wa vijana hawa unatambulika,maana si mara ya kwanza kufanya vizuri katika mpira wa miguu,kilimanjaro fc wamekuwa washindi katika mechi nyingi tena ushindi wa kishindo.nakumbuka mwaka jana wakali hawa waliichabanga tena timu hiyo ya kenya bao tano,na sasa nane safari ingine wakenya watafungwa kumi na mbili(12)ili kila mchezaji aondoke na goli lake kwenda kuonyesha nyumbani.
inafika muda itabidi ubalozi wa TZ hapa sweden wajaribu kuwapa motisha vijana hawa kwa japo kuhudhuria tu katika mechi zao na hata kuwapelekea maji au soda(haigharimu hata  kr 200).
wakenya wana bahati na suport kubwa sana toka kwa ubalozi na mashabiki wao,ni hivyo tu kwamba timu yao vibonde maana kama ingekuwa kali kama timu ya TZ sijui ingekuwaje.

mwaka jana balozi wao alihudhuria katika mechi ya fainali na kuishia kuona mara tano mipira ya magoli  ikitumbukizwa golini na vijana wa kili FC.na vijana wa kili FC wakiondoka na kikombe mbele ya macho ya balozi.
bahati mbaya sana mashabiki wa timu yetu hawakufika hata 20(aibu sana),na hakukuwa na kiongozi yeyote muhimu iwe toka ubalozini au hata kilimanjaro club(ZAM VP?) aliyehudhuria.

safari hii balozi wa kenya hakwenda akaingia mitini,lakini licha ya hivyo wakenya wagumu bwana na wanaipenda nchi yao wamehudhuria kwa wingi kuishangilia timu yao na kupokea mzigo wa magoli nane pamoja kwa uchungu(safi sana)
ushauri wangu kwa watani hawa wa jadi next time wabebe IKEA PÅSE kwa ajili ya kubebea magoli,na ushauri wa wa TZ jamani tujaribu kuwa wazalendo na kushangilia kilicho chetu,hata kama tuna ugomvi na baadhi ya viongozi wa club na chama,inapofika wakati wa mechi tuache hayo tuweke pembeni na kwenda kuwashangilia vijana ili kuwapa moyo.
hii kitu nilitaka kuandika siku nyingi sana tu lakini bahati mbaya sana sipati ushirikiano wa kutosha toka kwa wachezaji wa kili FC pamoja na viongozi wao,nimejaribu sana kuwaomba wanirushie picha na habari za matukio katika michezo naona wamegoma na  blog ya club kilimanjaroclub naona iko I.C.U ikipumulia mashine.  


1 comment:

  1. BABA MILTON sizani km ilo ni la kushangilia mi binafsi nimeshtuka kdg 8 kwa 1 that was not FOOTBALL at all mayb NETBALL na iyo timu si timu ni mfano wa timu huyo coach ajisalimishe mapemaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete