Thursday, 7 July 2011

KOFFI OLOMIDE&QUATER LATIN PARIS 2006



wakuu nairudia tena hii video,nishawahi kuweka huko nyuma.katika kipindi nilianza kuwa fan wa pappa mopao koffi olomide ni kipindi akiwa na hili kundi unaliona hapo,katika wachache nawakumbuka,kulikua na kerrosene,ferre gola,fally ipupa,montana kamenga,gibson butondolo,bill clinton kalondji (alijiunga toka kwa werra hakukaa) na wengine wengi.hao niliowataja walikua wanaimba na kupiga show pale mbele hakuna kuremba hakuna kuuza sura.nakumbuka katika tukio moja pale bongo montana kamenga kawahi kuja na defao enzi hizo siku aliyokuja na koffi alikoma kuringa.alipewa mick aimbe akaanza kuuza sura kama watu wamkumbuke.alinyanganywa mick na koffi live kwenye stage wakati kaimba labda mistari miwili ya nyimbo aliyotaka kuimba.

enzi hizo sebene likipata mashiko ni kwamba watu wanaliondoka kama wamepata roho mtakatifu(wananena kwa lugha)
siku hizi ukicheza sana bolingo huchelewi kuitwa shoga.
hii hobby tu bandugu ikitokea kwenye kupuliza moto watu wanaweza wakachochea kama vile wanapanda vilima vya turiani na baskeli.
mwisho mke/mke mtarajiwa anaishia kughairi kukaa mbezi na masaki anahamia mbagaraaaaaa rasmi.

endeleeni kukaa ushuani,si huku uswazi kajamb nani tunawangoja na usharobaro wenu.

na bahati mbaya tunavyojua kungoooja.laaaaaaaah

No comments:

Post a Comment