Monday, 16 May 2011 21:01 |
MAMIA ya watu kutoka Jamhuri wa Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na Rwanda baadhi yao wakielezwa kuwa ni maofisa wa serikali, jana walitua Samunge na kupata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila.Raia hao walitua Samunge kwa helikopta mbili za kukodi kutoka Arusha. Waliotangulia kufika Samunge ni Wakongo waliofika majira ya saa nne asubuhi.
Kwa mujibu wa maofisa wa Uhamiaji waliopo hapa Samunge, hati za kusafiria za Wakongo hao, zilionyesha kuwa baadhi ya yao ni maofisa wa serikali. Hata hivyo, hawakueleza nafasi zao serikalini licha ya awali kudaiwa kuwa mmoja wa wageni hao, alikuwa ni waziri. Ujio wa Wakongo hao, umekuja takriban wiki tatu tangu, Mama wa Rais wa DRC, Joseph Kabila kutua Samunge na kupata kikombe.Wakongo hao walifuatiwa na Wanyarwanda ambao pia walikuja hapa kwa ndege ya kukodi. Wagonjwa kutoka nje ya nchi ambao wamekuwa wakimiminika kwa wingi Samunge ni raia wa Kenya ambao hadi sasa idadi yao inafikia 150,000. Ujio wa marais, wafalme wawa siri Licha ya kuwepo taarifa za ujio wa marais kadhaa wa Afrika na wafalme kupata kikombe cha tiba Samunge, suala hilo bado ni siri. Msaidizi wa Mchungaji Mwasapila, Fredrick Nisajile licha ya kukiri kuwepo taarifa hizo za ujio wa marais na wafalme kutoka nchi za Kiarabu, alisema hawajui ni lini watatua Samunge."Wengi watakuja na tuna taarifa ila ukiniuliza ni lini hapo hatujui kama unavyojua hawa ni viongozi wa nchi, wana taratibu zao," alisema Nisajile. Babu: Sina mpango wa kusitisha tiba Mchungaji Mwasapila, jana alikanusha uvumi ambao umesambaa maeneo mbalimbali nchini kuwa atasitisha tiba kuanzia Mei 23, mwaka huu.Nisajile alisema Mchungaji Mwasapila hana mpango wa kusitisha tiba na ataendelea kuitoa... "Huu ni uvumi tu, hata sisi tumepigiwa simu kuulizwa kuhusiana na mchungaji kutaka kusitisha tiba. Ni uongo ambao wanasambaza maneno haya wana mpango wa kuharibu huduma hii." Ushuru mpya waanza Ushuru mpya wa Sh10,000 kwa kila gari linaloingia Samunge ulianza kukusanywa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Michael Lengume alisema wameanza makusanyo hayo mapya baada ya kusaini makubaliano na halmashauri kwamba watakuwa wakikusanya fedha hizo na kukata Sh4,000 za kijiji na nyingine watawakabidhi halmashauri. "Sisi tunakusanya zote halafu tunawapa zao 6,000 ambazo ni Sh3,000 za Halmashauri ya Ngorongoro na Sh3,000 za vituo vya uratibu magari," alisema Lengume MWANANCHI HIYO NDIO BONGO VIONGOZI WASHATENGENEZA ULAJI HADI KWA BABU.MWE NYEWE ANAYETOA TIBA WALA HATAKI TABU,500 TU ANATAKA ILI AWASAIDIE WAGONJWA WASIO NA FWEZA LAKINI WANAOIJUA HELA WASHAJITOKEZA NA KUWEKA CHAO MARA 20 ZAIDI YA KILE ANACHOPATA BABU.HAPO ANAYEUMIZWA NI MNYONGE TU HAKUNA KINGINE. |
Tuesday, 17 May 2011
Mamia ya Wakongo, Wanyarwanda watua Samunge
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment