Saturday, 21 January 2012

ALIYEKUWA MSANII NORA ARUDI KWAO


Brighton Masalu na Erick Evarist.
IKIWA imekatika takribani miaka mitatu ya ndoa bila mtoto, staa aliyewahi kung’ara kwenye uigizaji Bongo, Nuru Nassor Masoud ‘Nora’, amerudi nyumbani kwa wazazi wake, Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.
 Akizungumza na Risasi Jumamosi kwenye ‘spesho intavyuu’ juzi akiwa amesononeka, Nora alisema kwa sasa yuko nyumbani kwa wazazi wake akijishughulisha na biashara zake huku mumewe, Ally Masoud ‘Luqman’ akiwa Zanzibar kibiashara.
Nora ambaye kabla ya kuolewa na Luqman alitalikiwa na mumewe wa zamani, marehemu William Limbe ‘Ng’wizikulu Jilala’, alipobanwa juu ya usalama wa ndoa yake, alifunguka mengi yasiyotarajiwa.
Nora alisema mumewe amekuwa akimbana ile mbaya na kumzuia kufanya kazi ya sanaa kama awali.
Hata hivyo, Nora aliapa kuwa kama mumewe ataendelea na msimamo huo, yupo tayari kuachana naye kwani amechoka kuwa mke wa mtu.
Staa huyo aliyewahi kung’ara kwenye muvi za Sikitiko Langu na Dangerous Desire, aliendelea kumchana mumewe kuwa katika siku za hivi karibuni amekuwa akimpa vipigo mara kwa mara, jambo ambalo hakutarajia kukutana nalo kwenye ndoa yake.
“Kwa hali hiyo na mambo mengine ambayo siwezi kuyaanika, ndiyo maana nimechukua uamuzi wa kurudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko,” alisema Nora.

Hata hivyo, alipoona mapaparazi wetu wameshtushwa na kauli hiyo, aliwakata makali kwa kusema kuwa pamoja na yote hayo haina maana kwamba ndoa yake imevunjika.
Alipobanwa juu ya lini atarejea kwa mumewe mwenye maskani Magomeni, Dar, Nora aliweka ‘pleini’ kuwa kwa sasa anajishughulisha na biashara ya saluni na vipodozi huku akijipanga kurejea kwa kishindo kwenye tasnia ya filamu.
“Siwezi kusema ni lini nitarudi kwani nataka niwe bize kwanza na biashara na sanaa,” alisema binti huyo wa Kinyamwezi.
Waandishi wetu walipombana juu ya kutopata mtoto na jamaa huyo kwa muda wote walioishi, Nora aliweka mambo sawa kuwa suala la mtoto, yeye ndiyo hakutaka kuzaa.
“Sikutaka kuzaa kwani muda wangu haujafika japo nina mtoto mmoja niliyezaa na aliyekuwa mume wangu, marehemu Ng’wizukulu Jilala,” alisema Nora.

tokarisasij,mosi

No comments:

Post a Comment