Monday 10 May 2010

BIFU LA T.I.D NA HASHEEM THABIT

HASHEEM THABEET
TOP IN DAR

HASHEEM Thabeet ampiga mtama TID!
STREET FIGHT: HASHEEM THABEET VS. TID
ILIKUWA muda wa kama saa nane na nusu usiku. Siku ni Ijumaa tarehe Mei 7, 2010. Nilikuwa nimesimama nje kwenye parking karibu na mlango wa kuingilia Club Billicanas jijini Dar es Salaam nikitafakari nifanye makeke gani usiku huo. Nikiwa nimesimama kwa pembeni, nilimuona msanii wa Bongoflava maarufu kama TID akiingia club huku akiwa ameambatana na kimwana. TID alikuwa amevaa suruali jeans imepauka huku akining'iniza kitambaa (handkerchief) kwenye mfuko wa suruali wa nyuma. Alionekana akiwa high ready to have a good time in the club. Dakika kama 20 baada ya TID kuingia, nikaona Range Rover Sport nyeusi inaingia kwenye parking ya club. Kama sikosei number plates zake ni TSSS 101. Nikiwa nimevutiwa kuliangalia hili gari, nikaona vioo vimeshushwa na mchezaji wa basketball kule mtoni kwenye ligi ya NBA, Hasheem Thabeet, ndiyo anaendesha hiyo Rover. Akiwa amevaa kapero (cap) huku akiambatana na wapambe kama watatu, Hasheem alisalimiana na bouncers na washkaji wengine mlangoni na kuingia club.

Nikiwa naendelea kucheki vimwana wakali wakiingia club, mara naona TID anatoka kwa mwendo haraka kutoka ndani ya club. Nyuma yake namuona Hasheem anamfuata TID huku akiwa anaonekana mwenye hasira.

Mara Hasheem akampiga mtama TID akadondoka kwenye pavement karibu kabisa na mlango wa kuingilia club na kujipiga kisogo sakafuni. Wapambe na bouncers wakajaribu kumvuta Hasheem pembeni lakini Hasheem akaonekana mwenye hasira na kutaka kuendelea kumchapa TID.

Mpambe mmoja wa Hasheem akamwambia, "People are just looking at you cos you are the super star, achana na huyo **** (TID)."

Hasheem akamwambia TID "Mimi ni mtoto wa Sinza, usicheze na mimi ****mayo."

Wapambe wa Hasheem wakafanikiwa kumchukua Hasheem na kwenda naye kuelekea Ben Mkapa Towers, nadhani Savannah club.

Huku chini, TID akaanza kulia kwa sauti. He was kicking and screaming on the ground, obviously trying to create a scene aonekane kama kaumizwa sana na Hasheem. Msichana aliyekuwa na TID alibaki amesimama pembeni, looking sooo embarrassed huku TID akipiga mayowe.
Then TID got up and started running after Hasheem, demu wake alijaribu kumzuia akamsukuma kwa nguvu.

TID aliishia mpaka mbele kidogo ya eneo la kuingilia bar ya Break Point iliyo karibu na Billicanas na kukutana na askari polisi waliokuwa kwenye patrol.

Baada ya kuona Hasheem katoweka, TID alitimka zake kwenye eneo hilo na kuondoka mjini.

No comments:

Post a Comment