Friday 31 August 2012

WAREMBO WATANO WATINGA NUSU FAINALI REDDS MISS TANZANIA MORO


 Warembo watano waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi.…

 Warembo watano waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi.
 Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvisi Majaji, wakati wa shindano hilo.
 Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.
 Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Genevive Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.
 Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders, ambapo pia wadhamini wengine ni pamoja na mtandanowww.sufianimafoto.blogspot.com, Kampuni ya SPM:- Sufiani Photo Magic, Redd's, Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, B-Ze Hotel, Clouds Fm, Endepa, Gazeti la Jambo Leo na Simple & Easy Car.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.
 Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.
 Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea.
 Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Saxaphone kabla ya kuanza kwa shindano hilo.
 Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.
 Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora .
Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Saxaphone.

FLAVOUR WARM UP PARTY ON STOCKHOLM 1 SEPT 2012


Thursday 30 August 2012

FC KILIMANJARO YAICHAPA APOLLON SOLNA 5-2












MADAI T.I.D. ALITUMA WATU WAWILI KUMUUA ALIKIBA



Juzi kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Mohamed aka Top In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa kuwa alipanga njama za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.

Jana kupitia XXL ya Clouds FM, meneja wa Ali Kiba amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo.

Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua  Ali Kiba.

"Baada sasa ya taarifa hizo  kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale Ali Kiba anaishi wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kuchunguza hili na lile.

 Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatlia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata. 

Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hlo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndo anahusika.
Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."

Ameongeza kuwa TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi kupanga mpango huo wa kumuua Ali Kiba.

MSIBANI CONGO KINSHASA NA WENGE BCBG 6MAISON MERRE



HAPO ILIKUA NI MSIBANI WAKATI MNENGUAJI MMOJA WA WENGE B.C.B.G.ENZI HIZO  MONICA ALIPOFARIKI HUKO MONTREAL CANADA,MSIBANI IKAPIGWA STYLE ZOTE KUANZIA BILOKO,SOYON SERIEUS,MPUNDA,KISHA IKAMALIZIWA NA PELISA NGWASUMA,VIUNO NI VILIKATWA HAPO KAMA UNAVYOONA WAMAMA WALIKUA BIZZY KAMA WANALIPWA,HAKUNA KULIA NI UNALIA NA VIUNO TU,

WHAT I MISS FOR LUNCH TODAY!



                                     mbuzi choma,ugali na mbogamboga hasa majani ya maboga


                                                     hasa hii ya mkiani pale karibu na t**o


nyama choma tosha kwenye plate

bila kukosa majani ya maboga pembeni na kajiugali ka kishkaji

hii kitu haina recipe kwa leo,ila kukushauri uitafute hasa ukiwa nyumbani kule TZ utaipata mahali popote sehemu za kilaji,mimi nilikua napendelea zaidi pale sinza rombo green view,nyama yao ni balaa na pia nilikua nikiwa safarini kwenda home kule kitunda nilikua nastop pale kwa chota banana nao si mchezo kwenye kitengo hiki na kitimoto,na siku ingine ukitaka simple cheap and succulent nyamachoma basi pita pale opposite na mahakama ya ndizi mabibo,kuna jamaa pale container wanachoma nyama balaa na ni lunch tu,ukienda saa tisa unapiga olaa,wale wachaga unawatime saa 7 kamili unakuta mbuzi ndio inatiririsha utamu.nyama fresh kabisa kuanzia buku3 na ugali,kama ni mlaji haswa unakata ya buku 5 unakula mpaka unaacha


TUNDAMAN NEW VIDEO-DEM SIO

London Metropolitan University's visa licence revoked




A London university has been banned from teaching overseas students, leaving more than 2,000 undergraduates potentially facing deportation.
London Metropolitan University has had its right to sponsor students from outside the EU revoked, and will no longer be allowed to authorise visas.
Ministers have concerns over issues such as whether or not students are working instead of attending courses.
A task force has been set up to help students affected by the decision.
The UK Border Agency said it had "failed to address serious and systemic failings" identified six months ago.
As well as stopping the university, which has 30,000 students in total, from accepting new applications, losing the licence could also affect thousands of existing overseas students at the university.
The National Union of Students (NUS) said it could mean more than 2,000 students being deported within 60 days unless they found another sponsor.
'Panic and heartbreak'
The university's Highly Trusted Status (HTS) was suspended last month while the UKBA examined alleged failing, preventing it from being allowed to recruit overseas students.
Immigration Minister Damian Green said London Metropolitan University had failed in three particular areas:
  • More than a quarter of the students sampled were studying at the university when they had no leave to remain in this country.
  • A "significant proportion" of checked files found "no proper evidence" that the mandatory English levels had been reached.
  • Universities must know that students are turning up for their course and are not using a student visa to enter the country for work, but more than half of the records sampled suggested the university "just didn't know" whether students were turning up for classes or not.


A statement posted on the university's website on Wednesday read: "The implications of the revocation are hugely significant and far-reaching, and the university has already started to deal with these.
"It will be working very closely with the UKBA, Higher Education Funding Council for England, the NUS and its own students' union.
"Our absolute priority is to our students, both current and prospective, and the university will meet all its obligations to them."
Although there have been other suspensions, no other UK university has been fully stripped of its ability to recruit overseas students.
The NUS has contacted Prime Minister David Cameron and Home Secretary Theresa May to "express anger at the way that decisions have been made in recent weeks and to reiterate the potentially catastrophic effects on higher education as a £12.5bn per year export industry for the UK".
NUS president Liam Burns said: "This decision will create panic and potential heartbreak for students not just at London Met but also all around the country.
"This heavy-handed decision makes no sense for students, no sense for institutions and no sense for the country. This situation and the botched process by which the decision was arrived at could be avoided if international students were not included in statistics of permanent migrants."
Mr Burns added that UKBA "could very easily have said: 'Well London Met, if you're not capable of taking international students, you're no longer allowed to recruit any more" - instead of saying to all the current, legitimate students: 'You now have to leave the country'".
Help for students
Universities Minister David Willetts has announced a task force to help overseas students affected by the decision, which will include UKBA and the NUS.
He said: "It is important that genuine students who are affected through no fault of their own are offered prompt advice and help, including, if necessary, with finding other institutions at which to finish their studies."
A UKBA spokesman said it had been working with the university since it identified failings six months ago, "but the latest audit revealed problems with 61% of files randomly sampled. Allowing London Metropolitan University to continue to sponsor and teach international students was not an option".
"These are problems with one university, not the whole sector. British universities are among the best in the world - and Britain remains a top-class destination for top-class international students.
"We are doing everything possible, working with Universities UK, to assist genuine students that have been affected."

BBC

PICHA.HEKALU JIPYA LA MCHUNGAJI MAMA RWAKATARE



  Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare
 MC na mchungaji Haris Kapiga wa Clouds FM
 Mc Harris Kapiga akiwa kazini.
Watu wakijiachia
  Kabati la vyombo 
 Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.
Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi  la kifahari mjengoni humo
 Wakati wa msosi
 Mambo ya dressing table
Kitanda chake cha kulalia
---
 Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.
 
Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.

Images via Ruma Africa

NB:ISAACKIN
ENDELEENI KUPELEKA SADAKA NDUGU WAUMINI,MUDA SI MREFU MR ISAACKIN NTAINGIA KITENGO HICHO TUBANANE HUMO HUMO MAANA ......!

CHADEMA:TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAUAJI MORO





Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga kauli za Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zenye kulipotosha taifa kuhusu mashambulizi na mauji yanayoelezwa kufanywa na askari Mkoani Morogoro na badala yake kinataka uchunguzi huru ufanyike haraka kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act).

Kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani zina mwelekeo wa kulilinda Jeshi la Polisi ambalo askari na maofisa wake ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji, badala ya kuwezesha ukweli kuthibitika na hatua kuchukuliwa kwa wahusika.

Hivyokutokana na kujirudiarudia kwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola CHADEMA kinatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba ibara ya 33 ni mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu aingilie na kuwezesha uchunguzi wa kina.

Ikumbukwe kwamba tarehe 27 Agosti 2012 Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro lilifyatua risasi za moto na kupiga mabomu ya machozi wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kuelekea kwenye mkutano halali wa CHADEMA na wengine waliokuwa wakiendelea na shughuli zao eneo la Msamvu, hivyo kusababisha kifo cha raia mmoja asiye na hatia na kujeruhi wengine wawili.

CHADEMA kinaukumbusha umma kwamba kwa mauaji hayo na mengine katika maeneo mbalimbali nchini serikali inayoongozwa na CCM kupitia vyombo vya dola inaendelea kukiuka Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatambua kwamba uhai ni haki ya msingi kwa raia wote.

CHADEMA hakikubaliani na hatua zilizochukuliwa na Serikali mpaka sasa kuhusu tukio husika pamoja na maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani tarehe 28 Agosti 2012 ambayo kwa sehemu kubwa yametokana na taarifa zisizo za kweli kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi ambao ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji husika.

CHADEMA haina imani na timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi kuchunguza tuhuma za askari kufyatua risasi na mabomu ya machozi na kusababisha mauaji kwa kuwa tayari serikali na Jeshi la Polisi wametoa maelezo yenye kutofautiana kwa kiwango kikubwa na maelezo ya mashuhuda waliokuwepo na ushahidi wa picha za eneo la tukio.

Wakati Serikali na Jeshi la Polisi wakitoa maelezo kuwa marehemu alikutwa umbali wa mita 300 na kupelekwa hospitali na wasamaria wema, mashuhuda wameeleza wazi kuwa askari walifika jirani na eneo lake na ofisa mmoja akaonyesha ishara na ndipo risasi za moto na mabomu ya machozi yakafyatuliwa mojawapo kumpata marehemu na kudondoka.

Mashuhuda wote waliohojiwa wanaeleza kwamba bunduki ya polisi ndiyo ilielekezwa na kufyatuliwa kwa marehemu, maelezo pekee yanayotofautiana ni kuwa baadhi wameeleza kuwa ni bunduki ya risasi za moto na wengine wa wameeleza kuwa ni bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi.

Mara baada ya kudondoka gari hilo liliondoka na gari lingine la polisi lilifika likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia cha Mkoa ambaye alitoa amri ya gari lingine kumbeba Ali Hassan Singano (Zona) na kuondoka naye, hivyo si kweli kwamba matukio hayo yalitokea mbali na eneo bali pembeni ya meza ya muuza magazeti huyo karibu na barabara ya kwenda Iringa eneo ambalo polisi ilikuwa ikifanya mashambulizi.

Kauli zilizotolewa na Serikali kuwa Jeshi la Polisi lilizuia maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika Mkoani Morogoro kwa sababu ya sensa ya watu na makazi si za kweli kwa kuwa sababu pekee zilizotolewa ni ufinyu wa barabara na kuwa maandamano yalipangwa siku ya kazi. Ushahidi wa suala hili ni barua ya Jeshi la Polisi lenyewe ya 23 Agosti 2012 yenye Kumb. Na. MOR/A.25/1/VOL. II/202.

CHADEMA kinaujulisha umma kwamba Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro ndilo lililoacha kuheshimu utawala wa sheria na makubaliano yaliyofikiwa baada ya mazungumzo yaliyohusisha kikosi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kikiongozwa na Kamanda wa Operesheni za Jeshi hilo Simon Siro na hivyo kuwa chanzo cha mauaji yaliyotokea na madhara mengine kwa wananchi waliokuwepo maeneo yaliyorushiwa mabomu ya machozi.

Ikumbukwe kwamba awali CHADEMA kilipanga kufanya maandamano na mikutano katika Jimbo la Morogoro Mjini tarehe 4 Agosti 2012 na kuwasilisha taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Polisi wakakataa kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa kisingizio cha Sikukuu ya Nanenane, mgomo wa walimu na ratiba kugongana na ile ya mikutano ya CCM, sababu ambazo zilibainika kwamba hazikuwa na msingi wowote.

Baada ya mvutano na mazungumzo CHADEMA ilikubali kutii sheria na kuzingatia matakwa ya Jeshi la Polisi pamoja na kuwa yalitolewa kinyume cha Sheria kwamba maandamano na mkutano wa CHADEMA vifanyike mara baada ya siku ya kuanza kwa sensa tarehe 26 Agosti 2012 na CHADEMA ilipendekeza tarehe 27 Agosti 2012 ambayo Jeshi la Polisi liliikubali.

Polisi walifanya hivyo wakielewa ukubwa wa barabara za Morogoro na pia wakitambua kwamba ilikuwa ni siku ya kazi, hata hivyo tarehe 23 Agosti 2012 Jeshi la Polisi liliandika barua ya kueleza kwamba limetoa kibali cha mkutano (suala ambalo si mamlaka yake kisheria) na pia limekataza maandamano.

CHADEMA kikaamua kwa mara nyingine tena kurudi katika meza ya mazungumzo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, tarehe 24 Agosti 2012 ambapo polisi ilikubali maandamano ikiwemo ya watembea kwa miguu na kupendekeza njia mbadala na tarehe 26 Agosti 2012 mazungumzo yakaendelea kwa lengo la kukagua barabara.

Hata hivyo, kufuatia shinikizo la Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kinyume na Sheria ya Jeshi la Polisi ambayo imetoa mamlaka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya kuhusu taarifa za mikutano, polisi ikarejea katika msimamo wa kukataza mapokezi ya watembea kwa miguu na badala yake tarehe 26 Agosti 2012 bila sababu za misingi ya kisheria na zisizozingatia haki za kikatiba ikapendekeza kwamba yafanyike mapokezi kwa kutumia magari.

Maelezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa iwapo vyama vya siasa visiporidhika na mazingira kama hayo yapo mamlaka ya kukata rufaa yanapotosha kwa kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa hazijaweka utaratibu wa rufaa hivyo njia pekee ya kisheria ni kutumia mahakama.

Jeshi la Polisi lingeheshimu utawala wa sheria na mazungumzo lingeruhusu CHADEMA ifanye maandamano na kutoa ulinzi mpaka eneo la mkutano kwa muda mfupi badala yake jeshi hilo likaamua kutumia nguvu kubwa na kusababisha mauaji, barabara kufungwa kwa muda mrefu na kuathiri wananchi waliokuwa wakiendelea na kazi zao.

Iwapo wanachama na wananchi waliokuwa wamekusanyika kuwapokea viongozi na kuelekea kwenye mkutano wangekuwa wamekiuka sheria Jeshi la Polisi lingeweza kuwakamata kwa mujibu wa sheria, hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA aliyefunguliwa jalada mpaka sasa katika kituo chochote cha polisi kwa kudaiwa kukiuka sheria.

Kinyume chake Jeshi la Polisi ambalo likiwa kwenye mazungumzo lilikubali kuwa mapokezi yafanyike kwa msafara wa vyombo vya moto, lakini tarehe 27 Agosti 2012 likaamua kupiga mabomu ya machozi kwa wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika eneo la Msamvu wakiwasubiri viongozi bila hata ya kusubiri kuona iwapo yangefanyika matembezi ya miguu kuelekea eneo la mkutano au maandamano ya magari na vyombo vingine vya usafiri.

Kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kinyume cha sheria na kusababisha mauaji na kufunga barabara kwa muda mrefu kiliwafanya wanachama wa CHADEMA na wananchi kwa ujumla kutawanyika kuelekea eneo la mkutano na wengine kuingia barabarani kutembea kuelekea eneo la mkutano na hatimaye polisi walipoona wamesababisha hali hiyo wakaamua kulinda misafara hiyo mpaka eneo la mkutano hali inayodhihirisha kuwa uamuzi kama huo ungechukuliwa kutoka mwanzo yasingetokea madhara yoyote.

Kwa kuzingatia utofauti mkubwa baina ya maelezo yanayotolewa na Serikali na Jeshi la Polisi kuhusu matukio husika na ukweli halisi ulivyotokea, CHADEMA kinasisitiza kuwauchunguzi huru ufanyike kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania.

CHADEMA kwa mara nyingine kinaitaka Serikali inayoongozwa na CCM kurejea katika kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, ambacho kinatoa mamlaka ya Waziri mwenye dhamana na masuala ya Sheria kuanzisha Mahakama ya Kuchunguza Vifo hivyo (Coroner’s Court) katika maeneo ya serikali za mitaa kwa kushirikiana na Jaji Kiongozi.

CHADEMA kinaikumbusha Serikali kuwa, kufuatia kauli ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mawaziri Vivuli husika kueleza bungeni taarifa za mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola kwa nyakati mbalimbali, Waziri Mkuu na Mawaziri wengine waliahidi bungeni kwamba sheria hiyo itaanza kutumika kuchunguza vifo vyenye utata.

Katika muktadha huo uchunguzi wa kifo cha Ali Zona haupaswi kufanywa na timu ya polisi bali sheria hiyo sasa ianze kutumika.

Kwa upande mwingine, CHADEMA imeheshimu taratibu za maziko zilizopangwa na familia ambapo mwili wa marehemu ulisafirishwa jana tarehe 28 Agosti 2012 kwenda Mkoani Tanga kwa ajili ya maziko na CHADEMA kuwasilisha rambirambi zake za awali, taarifa zaidi kuhusu ushiriki kwa CHADEMA kwenye maziko zitaelezwa baada ya majadiliano yanayoendelea na familia.

CHADEMA kwa kuheshimu mazungumzo na utawala wa sheria kwa mara nyingine tena tarehe 28 Agosti 2012 CHADEMA kimesitisha Operesheni za Maandamano na Mikutano yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa rai iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ili kupisha kukamilika kwa zoezi la sensa ambayo imetokana pia na maelezo ya mamlaka zingine za kiserikali.

CHADEMA inatambua kwamba wakati maandamano ya CHADEMA yametolewa rai kuwa yasitishwe kupisha sensa, maandamano ya wagombea wa CCM kurudisha fomu za uchaguzi wa ndani ya chama chao yameachwa yakiendelea katika barabara kadhaa nchini bila kusitishwa kwa kisingizio hicho.

Aidha, wakati CHADEMA ikiheshimu mazungumzo na kusogeza ratiba yake mbele ya tarehe 26 Agosti 2012 mpaka tarehe 27 Agosti 2012 kupisha sensa hatua ambayo ilifanywa pia na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo ilitangaza ratiba yake kuendelea baaada ya tarehe hiyo.

Tume hiyo inaendelea na mikutano yake ya hadhara inayokutanisha wananchi katika kata za mikoa mbalimbali wakati huo huo zoezi la sensa likiendelea lakini kwa mikutano ya CHADEMA inaonekana kufanyika kwake ni kuingilia sensa.

CHADEMA inataka Serikali na Polisi kueleza iwapo matukio haya na mengine hayana mwelekeo wa ubaguzi na uhujumu wa vuguvuvugu la mabadiliko linaloendelea nchini kwa kurejea ukweli kuwa maisha ya wachache yanaweza kuwekwa mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

CHADEMA itaeleza hatua za ziada itakazochukua baada ya kupata ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu (post mortem) uliofanyika tarehe 28 Agosti 2012 na uamuzi wa Serikali kukubali au kukataa mwito wa kutumia Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) kuwezesha uchunguzi huru.

Imetolewa tarehe 29 Agosti 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi