Wednesday, 15 August 2012

KAJALA SHAVU DODO GEREZANI


 

Richard Bukos na Imelda Mtema
STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja Jumatatu iliyopita alizua  gumzo katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya kuonekana akiwa amenenepa tofauti na siku za nyuma alipokuwa akifikishwa mahakamani hapo kutokana na kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Risasi Mchanganyiko linakuhabarisha
Mapaparazi wa gazeti hili walimshuhudia Kajala akiwa na furaha huku mwili wake ukionekana kufutuka, hali iliyotafsiriwa kuwa ni kwa sababu ya kuzoea maisha ya gerezani.
Miongoni mwa watu walioshangazwa  na ubonge wa Kajala ni mkongwe wa filamu za maigizo hapa nchini, Muhsein Awadh ‘Dokta Cheni’ ambaye alishindwa kuvumilia na kuamua kumuuliza kulikoni.
“We Kajala mbona umekuwa bonge hivi, shavu dodo, hebu tupe siri ya mafanikio yako?” Dokta Cheni alimuuliza kwa utani, Kajala akacheka huku akielekea kizimbani na mumewe, Faraj Agustino kusikiliza kesi yao.
Mbali na Dokta Cheni, watu wengine waliofika mahakamani hapo walishangazwa na msanii huyo ‘kuumuka’ hivyo.
 Wakati akiwa katika chumba cha mahabusu, mmoja wa mapaparazi wetu alipata fursa ya kuongea na msanii huyo kwa kifupi ambapo alidai siri ya unene wake ni ugali wa dona na maharage ndivyo vinavyomtoa shavu.
Msanii huyo na mumewe Faraj  wanaotuhumiwa kwa kesi ya kutakatisha fedha haramu,Jumatatu iliyopita walipandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili ambapo hata hivyo kesi hiyo ilikwama kutokana na mmoja wa mawakili wa serikali anayesikiliza kesi hiyo kupatwa na udhuru hivyo kuahirishwa hadi Agosti 22, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

GPL

No comments:

Post a Comment