Wednesday, 29 August 2012

KAJALA,LULU WAPEKULIWA GEREZANI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MASTAA wawili wa filamu za Kibongo walioko lupango kwa tuhuma tofauti, Kajala Masanja na Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamedaiwa kupekuliwa na askari magereza na kukutwa na vipodozi katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam, Risasi Mchanganyiko  limeng’atwa sikio.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya gereza hilo, mastaa hao walipekuliwa Agosti 25, mwaka huu na kukutwa na baadhi ya vipodozi ambavyo haviruhusiwi kuingizwa gerezani humo.
“Lilikuwa ni zoezi la ghafla ambalo baada ya kufanyika Lulu na Kajala walikutwa na losheni wanazozitumia,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, mastaa hao ni warembo ambao wamezoe kila wakati kujiweka ‘sopusopu’, hivyo askari magereza walihisi watakuwa na vitu hivyo ukizingatia hivi sasa Kajala anazidi kupendeza pamoja na kwamba yupo gerezani.
“Vipodozi vile vilichukuliwa na wao kupewa onyo kwamba wasirudie kuviingiza tena gerezani la sivyo yatawapata makubwa zaidi,” kilimalizia chanzo chetu hicho.

GPL


No comments:

Post a Comment