Saturday, 10 September 2011

BABU AIBUKA TENA



 
Na Mwandishi Wetu
Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu’  (pichani) ameibuka tena hivi karibuni na kuweka wazi yanayoujaza moyo wake.

Akiongea na vyombo vya habari hivi karibuni kutokea kijijini Samunge, Loliondo, Babu alisema kuwa, ameongea na Mungu na ameambiwa kwamba, wagonjwa wanaokunywa tiba ya kikombe chake, hawatakiwi kunywa dawa nyingine yoyote ya ugonjwa uliowafanya wapate dawa yake.
Hapa alimaanisha kwamba, endapo mgonjwa anaugua TB, akipata kikombe chake hatatakiwa kunywa dawa nyingine kwa lengo la kuponya ugonjwa huo.
Kwa mantiki hii, Babu anakwenda pembeni ya matamshi yake ya kwanza ambapo aliwahi kuripotiwa akisema, wagonjwa wasiache kunywa dawa za hospitali hata kama watapata kikombe kwake.

Aidha, Babu Masapile alikwenda mbele zaidi pale aliposema kwamba, baadhi ya madaktari nchini wanamuonea wivu ndiyo maana wanasema dawa yake haiponyi.
Babu akahoji: “Mbona Wakenywa wanapona wengi sana na wanaongea vizuri kuhusu mimi?”
 
Akaendelea: “Tatizo Watanzania wengi hawana imani, na mtu akikosa imani dawa yangu haifanyi kazi.”
Aidha, Babu alisema kwamba, kwa sasa anapokea wagonjwa kiasi cha 40 mpaka 50 kwa siku moja, akasema tiba yake bado inatibu.

Hii ni mara ya tatu Babu kudai ameongea na Mungu. Mara ya kwanza ni pale alipoanza kutoa tiba mwaka 2007, akaja kuongea na Mungu mwaka 2010 ambapo alisema amepewa maelekezo mapya.

chanzo:GPL

Hundreds missing after ferry capsizes near Zanzibar


By the CNN Wire Staff
  • NEW: At least 259 people are rescued
  • NEW: At least 40 bodies are found, an official says
  • NEW: The ferry's manifest shows it was headed from the islands of Zanzibar to Pemba
  • Zanzibar is a semi-autonomous part of Tanzania
(CNN) -- Hundreds are missing after a ferry carrying more than 600 people capsized early Saturday near the coast of Zanzibar, authorities said.
At least 259 people have been rescued and 40 bodies found, said Mohamed Aboud, the Zanzibar state minister.
Divers and rescue crews are at the scene scouring the waters for survivors, he told CNN by phone from the site.
The ferry's manifest shows it was headed from the islands of Zanzibar to Pemba with more than 600 passengers onboard.
It was too early to tell what caused the accident, the state minister said.
No more information was immediately available.
Pemba and Zanzibar are the two main islands on the Zanzibar archipelago.
The two islands on the Indian Ocean are popular among tourists for their pristine sandy beaches.
Zanzibar is a semi-autonomous part of Tanzania

CNN

ABIRIA 250 WANUSURIKA NA KUOKOLEWA KTK AJALI YA MELI ZNZ


MELI ya Spice Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea bandari ya Malindi Unguja.
Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo zinaendelea hivi sasa.
Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku.
Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa.
Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki, lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.
Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi kama boti ziendazo kasi vimekwenda eneo la tukio kutoa msaada. Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helikopta yake kwenye eneo la tukio.
Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio. Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

MAESTRO VUMBI & DEKULA BAND LIVE@ LILLA WIEN BAR TODAY 10 SEPT



Dekula Band "Ngoma ya Kilo"
Place: Lilla Wien"Little Nairobi"
Date: 09-10 Sept.2011
Time: 21.00-01.00
Add: Swedenborgsg.20
Pendel: Södra Station

Wednesday, 7 September 2011

Mzee yusuph and jahazi cancelled instead african boogie night same day same lokal

Peter Jackson ▶ MZEE YUSSUF-JAHAZI MODERN TAARAB DEAR FRIENDS, SUN CITY SOUND FANS AND EVERYBODY, WE REGRET TO INFORM YOU THAT DUE TO THE REASONS BEYOND OUR CONTROL MZEE YUSSUF AND JAHAZI MORDEN TAARAB WILL NOT PERFOM IN STOCKHOLM, AS IT WAS PLANNED. THE SHOW HAS CANCELLED AND INSTED IT WILL BE A VERY SPECIAL NITE WHICH IS KNOWN AS" ALL AFRICAN NITE": THE VENUE : IS SAME LOCATION- SUBTOPIA- ALBY ADRESS:ROTEMANNAVĂ„GEN 10 TIME: 21:00-05:00 TICKETS: 100 KR LINE DJs:EZ FRANK(SOUND OF BLACKNESS) DJ: PUZZO(CURTAINS WORLD RECORDS) DJ: RICHIE(BEST OF BONGO FLAVA) DJ:PJ(SUN CITY SOUND) THIS SPECIAL NITE WILL GO WITH OLD SCHOOL,BEST OF BONGO FLAVA,TAARAB,KWAITO,BOLINGO,NDOMBOLO,ZOUK DANCEHALL,REGGE. I PROMISE YOU THAT NO ONE WILL REGRET TO ATTEND THIS NITE!! AND TIME IS UP TO 05:00 LATE MORNING !! DRINKS:AVAILABLE 4 REASONABLE PRICE!! TELL YOU ARE FRIENDS AND EVERYBODY !!

Monday, 5 September 2011

Wapenzi wa blog ya isaackin

Nawapa pole sana kwa kukosa uhondo wa eid na weekend kwa ujumla,hii yote ilitokana na mwanabloga kiongozi wa blog hii mr isaackin kupata ajali mbaya sana jumatano usiku wa eid mubaraq.kwa miujiza ya mola isaackin amekiepuka kifo si kwa ushujaa wake Ila kwa mipango ya mungu tu.ajali AMA tukio lilijiri katika mazingira ya ajabu sana na mpaka sasa limesababisha hasara kubwa sana. Basi hatutaongea sana kwani shughuli iko katika uchunguzi wa polis tutaendelea ku-update matukio Mara tu ntakapopata nafuu na kueleza kilichojiri. Asanteni na karibuni