Monday, 6 February 2012

MADAKTARI BINGWA MUHIMBILI NAO WAGOMA



Geofrey Nyang’oro na Florence Majani
WAKATI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikianza kazi ya kuzungumza na madaktari walio kwenye mgomo,  madaktari bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na walio katika Taasisi ya Mifupa (MOI) wamegoma.  Mgomo huo wa jana ulihusisha vitengo vyote huku wagonjwa waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo wakipewa taarifa za kuondoka katika wodi walimolazwa.

Azimio la mgomo huo lilifikiwa  katika kikao cha dharura kilichoitishwa na jopo la madaktari bingwa wakiongozwa na Dk  James Rwehabura ambaye ni daktari bingwa wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu.

  Habari za ndani kutoka katika kikao cha dharura cha wanataaluma hao, zilisema  uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha madaktari hao kilichoanza mapema asubuhi jana na kumalizika saa 6:00  mchana.  “Kwa pamoja tumekubaliana kuweka vifaa chini, hii ni kutokana na ukweli kuwa hali ya utoaji huduma katika hospitali hii ni mbaya huku taarifa za Serikali zikiwa siyo za kweli,” alidokeza mmoja wa madaktari bingwa.

Daktari huyo aliyekataa kutaja jina lake, alisema, “Tumekubaliana kugoma hadi hapo Serikali itakapotoa majibu ya madai yote yaliyowasilishwa na jumuiya ya madaktari inayoongozwa na Dk Stephen Ulimboka kwa Serikali.”  Jumuiya hiyo iliwasilisha madai mbalimbali likiwamo la kuitaka Serikali kupeleka vifaa na dawa katika hospitali za Serikali ili madaktari hao waweze kutoa huduma bora kwa jamii. 
Pia, madaktari hao walitaka kusitisha safari za vigogo kwenda kutibiwa nje kwa magonjwa yanayotibika ndani kwa kile walichodai, hali hiyo inachangia wao kudharauliwa na pia kuzorotesha jitihada za Serikali katika uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa madaktari hao.

 Kwa nyakati tofauti, madaktari hao walibainisha sababu ya mgomo wao na kudai kuwa, kikubwa ni mazingira magumu ya kazi.   Daktari mwingine ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini alisema, licha ya mishahara na posho ndogo, lakini mazingira ya kufanyia kazi yamekuwa magumu mno.  

“Tumeshaamua , ‘tools down’ hospitali haina kitu, hata ‘mask’ hakuna badala yake tunavaa gozi tunapofanya upasuaji, acha hiyo, hata nyuzi za kushonea wakati wa upasuaji hakuna,” alisema daktari huyo.  Daktari huyo alisema, hawawezi kufanya kazi katika mazingira hayo kwa sababu  yatawasababisha kuwa na utendaji mbovu na baadaye taifa kuwalalamikia.

Alisema hapa nchini madaktari bingwa ni wachache, kwa hiyo kitendo cha wao kufanya kazi peke yao bila wasaidizi, yaani madaktari wa mafunzo na wale wanaomaliza, wanaelemewa na mzigo wa kazi.  Dk Henry Mwakyoma, Mhadhiri Mkuu wa Chuo cha Udaktari Muhimbili, (MUHAS) ambaye hakuwapo katika kikao hicho cha dharura alidai kuwa, yeye kama mhadhiri hajagoma, lakini alikiri kuwapo kwa mazingira magumu ya kazi.

“Mpaka sasa hatujalipwa mishahara ya mwezi uliopita, halafu kazi yetu ndiyo kama hii tunatakiwa tufanye utafiti, unategemea tutafanya kazi kwa umakini kweli? Tutawafundisha madaktari kwa umakini?” alihoji Dk Mwakyoma. 

Mwakyoma alisema, Serikali haiwezi kudai kuwa haina fedha za kutosha wakati imetumia mamilioni ya shilingi katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru na uchaguzi wa Igunga.   Alisema ni vyema Serikali ikajipanga na kuamua kushughulikia masuala ya madaktari kwa hekima kwani kukaa kimya bila kutoa suluhu ni sawa na kufanya ushindani usio na maana.
 Hata hivyo, Ofisa Habari Mwandamizi wa MNH Aminael Aligaesha alisema jana jambo hilo lilikuwa likishughulikiwa kwani vipo vikao vinavyoendelea.  

Wagonjwa watimuliwa wodini
Wodi mbalimbali hospitalini hapo zilitawaliwa na vilio kutokana na wagonjwa na ndugu za wagonjwa kupewa taarifa za kuondoka katika eneo hilo mara moja, kutokana na mgomo huo wa madaktari. Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi ya Sewahaji, Sadick Dimoso (35) mkazi wa Morogoro alisema hali sasa MNH ni mbaya. 

“Tumeambiwa tuondoke wodini bila ya kuruhusiwa na daktari, hii ni hatari tena wanasema tuondoke tukakae huku hadi wiki mbili ndio turudi kuangalia,” alisema Amina Ramadhani, aliyekuwa akisubiri kufanyiwa upasuaji wa jicho.  Alisema hatua ya kutakiwa kuondoka hospitalini hapo imekatisha matarajio yao ya kuendelea kuwa hai na kuitaka Serikali kufanyia kazi madai ya madaktari.

Wakati kundi la watu wengine wakililia huduma hosptalini hapo, baadhi ya ndugu za wagonjwa waliingia katika mgogoro na walinzi wa wodi hiyo ya Sewahaji wakitaka waandishi wa habari kuingia wodini.

Vikao vya Kamati Wakati hayo yakijiri, vikao baina ya madaktari na Kamati ya Kudumu ya Huduma za Bunge, viliendelea jana katika ofisi ndogo za Bunge huku taarifa zake zikiwa ni  siri.


chanzo:mwananchi

Saturday, 4 February 2012

Europe freeze hits transport hubs

A Bosnian man walks near a frozen tram in the Bosnian capital of Sarajevo, on February 4 The Bosnian capital Sarajevo has ground to a halt amid the big freeze

Freezing weather has hit transport hubs across Europe, closing airports, blocking roads and halting trains.
London's Heathrow cancelled 30% of Sunday's flights, and dozens of flights were delayed at Amsterdam's Schiphol.
Transport hubs in Central and Eastern Europe have been forced to close amid the biggest freeze in decades, which has claimed more than 200 lives.
Bosnian officials have declared a state of emergency in Sarajevo, where snow has paralysed the city.
In Serbia, a state of emergency is in place across much of the country.
Thousands of people are said to be trapped in their homes across both countries, and many travellers have been stranded.
"I've been waiting here two days and we don't know what we will do," said Turkish tourist Ducim Tahroglu, waiting at Sarajevo airport.
Ukraine has been hit hardest by the weather, recording more than 100 deaths so far.
Forecasters predict the freeze will ease in Ukraine, though parts of the country will still be enduring temperatures as low as -19C.
The Siberian weather system has brought heavy snow and temperatures plummeting to below -30C in parts of Central and Eastern Europe.
The spike in energy demand forced Russian gas supplier Gazprom to reduce its deliveries to Europe over the past few days.
The firm said it could fulfil the demands of all of its customers, but insisted that supplies were now back to normal levels.
The freezing weather is now moving westwards, with most of the UK expecting snow overnight on Saturday.
In Italy, canals in Venice have begun to freeze over, and the capital Rome has seen its most severe snowfall in more than 25 years.
The Netherlands marked temperatures of -21.8C in the town of Lelystad on Saturday, the lowest recorded in the country for 27 years.
Motorist associations reported hundreds of miles of traffic jams across Belgium and the Netherlands as the first snow fell on Friday.

BBC

JK ATUA JIJINI MWANZA TAYARI KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA UHURU


 Jk akishuka kwenye ndege alipowasili uwanja wa Ndege wa Mwanza leo jioni
  Rais Kikwete akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mwanza  Injinia Evarist Ndikillo baada ya kuwasili Uwanja wa ndege jijini Mwanza leo jioni.
 Rais Kikwete akifuatana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza  Mabina wakati alipowaisli jijini Mwanza leo
 
  Rais Kikwete akiwasalimia wanachama wa CCM baada ya kuwasili jijini Mwanza
Katibu wa NEC, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mabina na Katibu wa CCM  Mukama wakisahuriana jambo kwenye Uwanja wa Ndege jijini mwanza wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Friday, 3 February 2012

Rough weather causes train chaos in Stockholm

Rough weather causes train chaos in Stockholm

Train chaos swept railways south of central Stockholm on Friday morning, after an overhead line fell onto the tracks between Stockholm and the country’s south.

”It is effectively a cut in the bloodstream when it stops south of Stockholm. There are only two ways in to the city centre, and the traffic has had to go northwards,” Maricka Berggren of train company SJ told the TT news agency.

The collapsed line, most likely due to rough weather, caused one train to get stuck in a tunnel at 6.30am for three hours, until emergency services and police could release them.

Between 20 and 25 people were stuck on the early morning train for hours, according to Dagens Nyheter (DN) newspaper, and many more were stuck on platforms in the freezing cold.

Örjan Wallin was one of those trapped, and claims to have been stuck for three and half hours on the cold train.

“It got a little chilly on the train, but we all sat their peacefully and read the paper or typed on mobile phones,” he told DN.

Other commuters were not as calm.

“This is the worst train system in the world north of Bangladesh,” grumbled one commuter to TT news-agency.

“We’re used to it”.

Trains travelling south of the capital were delayed by as much as two hours after the incident, many commuters opting to move northwards out of the city instead of taking their chances waiting for the south bound train lines to reopen.

Information boards were also out of order, and travellers had trouble connecting with SJ to query about the delays.

In a separate incident, rail traffic passing Nässjö was delayed because of a fire in an industrial building, which created a massive explosion risk due to gas containers inside the building.

This potential hazard halted trains heading towards Malmö and Gothenburg. Rescue services however, extinguished the flames quickly.

Meanwhile, the Swedish Transport Administration (Trafikverket) on Thursday released a statement indicating that 87.1 percent of the country’s passenger trains ran on time over the previous year.

The statement also said that 76.2 percent of the country’s freight trains were on time in 2011.

37PEOPLE DIED IN SOUTH SUDAN UNITY STATE PEACE TALK

 

map
At least 37 people have been killed in South Sudan during a shoot-out at a peace meeting aimed at ending recent violence, officials said.
Officials from three states and the UN had met for talks in the remote town of Mayendit in Unity state in an effort to reduce inter-ethnic tensions.
The talks were called after a series of clashes, including one in which 74 people were killed earlier this week.
Thousands of people have been displaced in the violence.
According to the UN, the fighting took place when four trucks of gunmen arrived at the meeting after a row broke out, and began to shoot indiscriminately.
The gunmen included policemen from different units, soldiers, bodyguards and armed wildlife officials, according to AFP news agency.
Many others were wounded in the confrontation, including a UN staff member.
Correspondents say the lack of security in South Sudan, which became independent last July, is one of its greatest challenges.
Hundreds of people have also been killed in a series of tit-for-tat cattle raids in Jonglei state in recent weeks.

source:bbc

CHADEMA WAIJIBU CCM JUU YA POSHO YA WABUNGE


Kauli ya CCM juu ya nyongeza ya posho za vikao kwa wabunge ni ya kinafiki, haionyeshi uongozi thabiti na inalenga chama tawala kujikosha kutokana na hasira ya umma dhidi ya viongozi waandamizi wa chama hicho na wabunge wake kutaka nyongeza ya posho za vikao kinyemela.
Aidha, kauli hiyo ni muendelezo wa kauli za CCM za kujikosha mbele ya umma baada ya wananchi kupinga maamuzi ya serikali inayoongozwa na chama hicho katika masuala ambayo chama hicho kilikuwa na taarifa nayo kabla lakini kikashindwa kutoa muongozo unaostahili kwa serikali kama ilivyokuwa kwenye suala la kupandisha kupindukia kwa ushuru wa mafuta ya taa na kuongeza bei na gharama za maisha kwa wananchi wa kipato cha chini au kuhusu malipo ya fidia kwa Dowans.
Kauli kwamba ‘CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na mchakato wa swala la nyongeza ya posho za vikao kuliangalia upya na kutumia busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa’ inadhihirisha kwamba kimsingi chama hicho kimepoteza uwezo wa kuwa chama tawala.
Kauli kama hii ni kama agizo lililotolewa na Kamati Kuu ya CCM katika kikao chake cha tarehe 31 Agosti 2011 ya kutaka serikali ipunguze bei ya mafuta ya taa baada ya kuona wananchi wanaungana na msimamo wa CHADEMA uliotolewa bungeni na wabunge wake wakati wa kupitishwa kwenye muswada wa sheria ya fedha mwezi Juni 2011 na kujadiliwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini tarehe 15 Julai 2011.
Hata hivyo mpaka sasa agizo hilo ambalo limetokana na kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete halijatekelezwa hali ambayo inadhihirisha ulegelege wa CCM na serikali yake katika kusimamia masuala ya msingi ya taifa hali ambayo athari zake zinathibitika hivi sasa katika mjadala huu wa posho za vikao ambapo ombwe na uongozi linaonekana bayana katika chama hicho na serikali.
Kauli ya CCM ya kumpongeza Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho kwa kushindwa kuonyesha uongozi na badala yake kutupa mzigo wa wabunge kwenye suala ambalo kwa mujibu wa sheria Rais ndiyo mwenye mamlaka nalo ni ishara ya CCM kulea misingi ya kutowajibika miongoni mwa viongozi wakuu wa serikali na chama hicho.
Iwapo CCM ingekuwa na dhamira ya kweli ya kukataa posho za vikao ingefanya maamuzi ya kukataa kupitia vikao vya chama hicho vya kamati kuu na halmashauri kuu ambavyo viliongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete kwa nyakati mbalimbali wakati ambapo mjadala wa posho za vikao ukiwa tayari umekolea katika taifa baada ya CHADEMA kuibua suala husika ndani na nje ya bunge kuanzia wakati wa bunge la bajeti kupitia pia maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.
CHADEMA inaitaka CCM kama kweli inajali maslahi ya wananchi kufanya maamuzi ndani ya vikao vya chama hicho na kuandaa mapendekezo kwa serikali ya kufuta posho zote za vikao kwenye mfumo wa utumishi wa umma kama ilivyoelezwa katika ilani ya CHADEMA ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Mpango wa Taifa wa miaka mitano uliopitishwa na bunge mwaka 2011.
Aidha, badala ya kumpongeza Rais Kikwete kwa kauli iliyotolewa na ikulu ya kuhamisha lawama kuhusu suala hilo kwa wabunge, CCM itoe mwito kwa Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho kutoa kauli yake mwenyewe ya kufanya uamuzi wa kufuta posho za vikao katika mfumo wa utumishi wa umma na kutoa kauli ya wazi ya kukataa nyongeza ya posho za wabunge.
Pia, CCM badala ya kutaka tu wabunge kwa ujumla kutafakari ieleze inachukua hatua gani kwa viongozi wa serikali na bunge wanaotaka na chama hicho kunukuliwa na vyombo vya habari wakieleza kwamba Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho kuwa amebariki nyongeza ya posho hizo na hivyo kukosekana kwa uwajibikaji wa pamoja katika serikali na chama hicho.
Kushindwa kwa CCM kuchukua hatua za kichama dhidi ya viongozi hao ambao ni wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kunadhihirisha kwamba pamoja na kuwa Rais Kikwete hajasaini masharti mapya ya kazi za wabunge ameshakubaliana nao kinyemela kuhusu kuanza kutoa nyongeza ya posho za vikao; kinyume na hapo kauli za CCM zitaendelea kudhihirika kuwa ni za kinafiki na za kujikosha.
CHADEMA inaendelea kusisitiza kauli yake kwamba ongezeko la posho ya vikao lilofanyika linapaswa kusitishwa kwa kuwa limefanyika kinyume na taratibu na pia halina uhalali wowote kimantiki na halijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla; nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni haramu (Illegitimate).
Aidha, kauli iliyotolewa kwamba nyongeza hiyo ya posho za vikao ni kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha mkoani Dodoma haina ukweli, wala mantiki na ina mwelekeo wa upendeleo.
Nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni matumizi mabaya ya madaraka na ni dharau kwa walipa kodi wanaohangaika na kupanda kwa gharama za maisha na athari za ubadhirifu wa fedha za umma. Ni udhaifu kufikiri kwamba suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha ni kuongeza posho za kikao; tatizo la kupanda kwa gharama za maisha linapaswa kushughulikiwa kwa kuchukua hatua dhidi ya matatizo ya kiuchumi katika nchi ili kuweza kuwa na tija kwa wananchi wengi ambao ni waathirika zaidi wa kupanda kwa gharama za maisha kuliko wabunge.
CHADEMA inarejea kuukumbusha umma kwamba Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Administration Act) ya mwaka 2008 kifungu cha 19 kinataja aina ya posho ambazo zinaweza kutolewa kwa wabunge kama ambavyo Rais ataeleza kwa maandishi. Katika kipengele (d) sheria imetaja orodha (i) mpaka (iii) ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa za usafiri, kujikimu na wasaidizi. Katika orodha hiyo hakuna Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja ambayo kamati ya wabunge wa CHADEMA tunataka ifutwe mara moja kama sehemu ya mchakato wa kubadili mfumo mzima wa malipo ya posho kwa watumishi wa umma.
Kifungu 19 (d) (iv) kimempa mamlaka Rais ya kutoa posho zingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu hiki kimetoa mwanya wa kutolewa kwa waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa tarehe 25 Oktoba 2010 wenye kumbukumbu na. CAB111/338/01/83 masharti ya kazi ya mbunge ambao umeeleza viwango vya posho mbalimbali ikiwemo kutoa posho ya vikao (Sitting Allowance).
Hivyo, badala ya Rais Kikwete kukwepa wajibu huo wa kisheria na kuhamisha mzigo kwa wabunge anapaswa yeye mwenyewe kufanya uamuzi wa kukataa nyongeza ya posho za vikao na kufuta posho za vikao katika mfumo mzima wa utumishi wa umma kama ilivyopendekezwa na CHADEMA pamoja na kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Izingatiwe kwamba uchumi wa nchi hivi sasa unasuasua, serikali ina hali mbaya ya fedha kutokana na kupungua kwa kiwango cha fedha kinachopatikana katika kodi na washirika wa kimaendeleo ukilinganisha na mahitaji ya bajeti; na hivyo kukopa kibiashara kwa ajili ya kuziba nakisi iliyopo.
Kupungua kwa uzalishaji, kiwango cha fedha pamoja na kuongezeka kwa ubadhirifu katika matumizi ya rasilimali za umma kunachangia katika mfumuko wa bei hali inayohitaji mpango wa dharura wa kunusuru uchumi wetu ukaohusisha pamoja na mambo mengine kubana matumizi ya serikali.
CHADEMA kwa kurejea tamko la mwanzo wa mwaka 2012 lililotolewa na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa ambalo limetaka kipaumbele kiwe ni kunusuru uchumi wa nchi na kupanda wa gharama za maisha kwa wananchi, tulitarajia kwamba CCM na serikali yake watoe kwa umma mpango wa kukabiliana na hali hiyo badala ya kurushiana mpira kuhusu nyongeza ya posho za vikao huku mwelekeo wa uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ukiwa kwenye hali tete na nchi ikiwa kwenye migogoro ya kijamii kuhusu maslahi ya madaktari, wanafunzi na makundi mengine katika jamii.
CHADEMA inasisitiza msimamo wake kwamba posho za vikao zifutwe kwa kuzingatia kuwa Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 imeeleza kwamba lengo la msingi ni kuondoa posho za vikao (sitting allowance ) hatua ambayo itaambatana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, wajibu ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki; uamuzi ambao utawezesha pia kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo.
Imetolewa tarehe 02/02/2012-Dodoma na:
John Mnyika (Mb)
          Mkurugenzi wa Habari na Uenezi