Thursday, 18 September 2014

TANZANIA DAY - STOCKHOLM, SWEDEN, 27 September 2014.


Tafadhali sana chama na jumuiya ya watanzania Sweden wanomba mfikishe hizi habari kwa watanzania wote mahali popote walipo. Tupo pamoja na kufika kwenu ni furaha yetu, kujumuika nasi ni njia moja ya kutuwezesha kuimarisha maendeleo na misingi endelevu. Naambatanisha mfano wa freeticketi baada ya kujiandikisha.
 
natanguliza sana shukrani
Tengo Kilumanga
Mwenyekiti
 

TANZANIA DAY - STOCKHOLM, SWEDEN
27 SEPTEMBA 2014

MKUTANO WA WATANZANIA SWEDEN WA

KUMKARIBISHA

BALOZI MPYA WA TANZANIA


UBALOZI WA TANZANIA  UNAPENDA KUWAARIFU KWAMBA
BALOZI MPYA WA TANZANIA, MHE. DORA MSECHU AMEWASILI RASMI SWEDEN.


TAREHE 27 SEPTEMBA 2014 KUTAKUWA NA MKUTANO MAALUMU WA KUMKARIBISHA
MHE. BALOZI MSECHU. 

MKUTANO HUU UTAFUATIWA NA BURDANI YA SIKU YA WATANZANIA ("TANZANIA DAY") ILIYOANDALIWA NA JUMUIYA YA WATANZANIA SWEDEN (TANZANISKA RIKSF?RBUNDET)


SHUGHULI ITAFANYIKA KATIKA
UKUMBI WA SHULE  YA BERGSHAMRA, HJORTSTIGEN 1, BERGSHAMRA, SOLNA
KUANZIA SAA KUMI ALASIRI (1600HRS)

MKUTANO RASMI WA KUMKARIBISHA BALOZI UTAANZA NA KUFUATIWA NA BURDANI YA CHAKULA, VINYWAJI NA MUZIKI.

WATANZANIA MLIOPO SWEDEN MNAOMBWA MJITOKEZE KWA WINGI KWENYE SHUGHULI HII YA KUWA PAMOJA NA KUMKARIBISHA BALOZI WETU MPYA.

No comments:

Post a Comment