Saturday, 26 July 2014

MAMBO YA ALIKIBA NA DIAMOND

Na Sifael Paul

Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).
Staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba.
Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.…
Na Sifael Paul
Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).
Staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba.
Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo akatiririka:
“Nilikuwa nayo kipindi fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima wa kuwa nayo.
“Kuna kipindi alinikosea kwa sababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ule Wimbo wa Single Boy, jambo ambalo halikuwa kweli. Halafu akasema mimi ndiyo nilimfuta.
Staa wa muziki Bongo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
“Diamond alinikosea kwa sababu kutokana na mimi ndiye nilifanya wimbo wake wa Lala Salama ambao upo kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichoniomba nifanye nilifanya kwa mapenzi yote na mimi namsapoti kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri, sikatai anaimba vizuri, sijui ukisema amekopi, mimi sijamaindi wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya nikaonekana mimi sifai, siko hivyo mimi.
“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Ali Kiba. Wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nilimfuta kwenye wimbo wangu wa Single Boy lakini mimi wala, shahidi yangu ni produyuza Manecky (AM Records) kwani ndiye alitengeneza ule wimbo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael 'Lulu'
“Sikuwahi kwenda studio na Diamond, sikuwahi kufikiria kufanya wimbo naye. Ila alinipigia simu baada ya ule wimbo wa Single Boy kuvuja. Akaomba afanye na mimi, akanipa hadi idea (wazo) ya video, nikamwambia nimeshafanya na Jaydee (Judith Wambura).
Nikamwambia itapendeza zaidi tukifanya wimbo mwingine kwa sababu hii tukifanya mimi na wewe haita-make sense (haitaeleweka), inapendeza ikiwa single boy na single girl, hicho ndicho kitu nilimjibu.
“Baada ya kama wiki moja nikasikia kwenye mablog, nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta Diamond kwenye ule wimbo wakati yeye ndiye aliyenifuta katika wimbo wake, shahidi prodyuza wangu KGT.
“Kutoka hapo nikaona hakuna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika wimbo wake. Mimi siyo shabiki wa Diamond ni shabiki wa muziki mzuri. “Kuna watu wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma.
“Niliambiwa alisema vitu vingi, mara nilikopa fedha benki ili nimalizie nyumba na mambo kama hayo so siwezi kufanya naye kazi.” Baada ya Kiba kumchakaza, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond naye alijibu mapigo bila kutaja jina la Kiba ambapo aliandika: “Tatizo lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke…Wakati mwenzako nawaza kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini kwetu.”

Hata hivyo, baada ya hayo yote kuliibuka madai kwamba mbali na ishu za muziki, mastaa wa kike wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu wanahusishwa kwenye gogoro hilo kisa wivu wa kimapenzi hivyo ishu hiyo bado ni mbichi. Tusubiri mwisho WAKE!

GPL

No comments:

Post a Comment