Tuesday, 4 December 2012

UNIQUE MODEL 2012 NDANI YA KIVAZI CHA KUOGELEA




NGWASUMA-VUTA NIKUVUTE TUVUTANE,BURULA NIKUBURULE TUBURULANE-UJUMBE MKALI SANA HAPA



huwa najisikia raha sana mara kwa mara nikisikia nyimbo hii,ujumbe umetulia na kuna ukweli ndani yake,nafurahi siku hii wazee wa ngwasuma wanaimba kiswahili mwanzo mwisho na sie maganga tunaelewa wanachoimba.
na katika hilo ndio nakuja kugundua kwamba hawa jamaa kumbe walikuwa wanapiga nyimbo kali nzito na zenye ujumbe mkali hapo nyuma,sema usipokuwa unaelewa we unasubiri ichanganye ucheze yaishe.
hapa kuna ujumbe ambao mara kwa mara huwa unanirudia akilini.hasa pale wanapoimba kwamba "usilinganishe riziki na uhai wa bin adamu,uhai wa bin adamu ni bora kuliko riziki,ndugu yako anapofanikiwa huanza kumchukia na kujipa uwezo wakudhuru maisha yake" 
na pale Patcho anapoimba
" kupata kwako isiwe sababu ya kunyanyasa wenzio,mafanikio yako isiwe sababu ya kunivurugia ndoa yangu wee,hakuna aliyekamilika duniani,hakuna aliyekamilika sisi wote mareehemu watarajiwa,wako wapi Mwalimu Nyerere na Mobutu Seseseko?itakua sisi wapangaji,hakuna aliyeweza ishi na tamaa,anayetembea kwa miguu ndoto yake kununua baskeli,aliye na baskeli anatamani pikipiki mwenye pikipiki anatamani corolla,kila mwenye corolla anataka vitara,kila mwenye vitara anatamani apate pajero,mwenye pajero anatamani VX,kila mwenye VX anataka apate Hummer kila mwenye Hummer atatamani ......"and so on
" and on.

mashairi hayajaishia hapo kuna Kabeza anampokea Patcho na yeye anaimba yake ingawa siku hizi hayuko vizuri upstair kwa ajili ya hao hao bin adamu wamemtengeneza lakini kumwaga mashairi kama kawaida.

acha pale mwisho ikichanganya unapokuja kumsikia Kitokololo"kuku" na G7 wanapokucheza tingisha tingisha mayemba,inauma inai.... na mwisho utamu wa vanilla eeeh na nzombo na matembele.raha tupu

TUPENDANE WAJAMAA WENZANGU,SIE WAPANGAJI TU HAPA DUNIANI HASA SVERIGE..

Monday, 3 December 2012

Work must come before reunification: minister

Work must come before reunification: minister


Sweden's Migration Minister Tobias Billström wants more migrants to get jobs before their families can follow them to Sweden, but he may face an uphill struggle to convince his government partners to tighten up current family reunification rules. 
 Two years ago, a law came into force requiring immigrants to have a job and somewhere to live before applying to have their families follow them to Sweden.

In 2011, 366 applications by immigrants to join a family member in Sweden were rejected because the person in question was not working.

By 2011, less than half that number were rejected, reports political newspaper Riksdag & Department (RoD) after looking at Migration Board (Migrationsverket) figures, something which doesn't sit well with Billström.

”Far too few people are subjected to this requirement if you look at it in relation to the large number of people who come to Sweden through family reunification," he told Sveriges Radio (SR).

"That’s why the self-sufficiency requirement should be thoroughly examined."

Prime Minister Fredrik Reinfeldt stood behind his minister on Monday.

“Tobias Billström feels that exceptions to the law have become too widespread,” Reinfeldt told the TT news agency.

But other members of the government coalition think the exceptions were made for good reason.

“People who are issued an exception to the rules are mostly minors. They have been living in the very situation from which their parents fled,” Christian Democrat MP Emma Henriksson, who sits on the parliamentary committee on social security, told TT.

"We’re talking about Somalia but also Syria.

"It is important to us that we don’t propagate policies that keep families apart. Parents and children should be together.”

The government says the law was meant to provide an incentive for immigrants to find work, a claim Reinfeldt reiterated on Monday.

"We think it’s important that immigrants are included in our labour policy. It is also a way for Sweden to prepare for the many relatives we are expecting,” said Reinfeldt.

Earlier this year, Sweden scrapped a requirement that Somali immigrants show documentation to prove family ties. The government instead opened the door for DNA testing.

"Somalis are one example,” Reinfeldt said.

"But in general this is related to our high level of asylum seekers. And it will apply to unaccompanied refugee minors who at a later date want their families to follow.”

The prime minister seemed aware that his Billström might face some opposition for his call to make it hard to claim an exception to self-sufficiency requirements.

“We have to discuss this with our coalition partners and also, further on, with the Green Party,” Reinfeldt told the TT news agency.

After the last election, the centre-right Alliance government struck a deal with the opposition Green Party on immigration policy

The agreement was a way to exclude the anti-immigration Sweden Democrats from having any chance to vote against the minority government in parliament on issues related to immigration policy.

The deal with the Green Party has already forced the government to make certain compromises.

Green Party migration policy spokeswoman Maria Ferm said on Monday that her party would not get involved in changing the current reunification rules.

“It is a human right to be reunited with your family if you have escaped war or conflict,” she told TT.

She also said the proposal could damage Sweden’s efforts to help newly-arrived immigrants integrate.

"It’s counter-productive. If people have to worry constantly about their family and whether they are alive or dead, it is difficult to get into a new society, learn a new language and find a job," said Ferm.

TT/The Local/at

WABONGO NA FITNA FITNA!

SOMA HAPO


                                      MISS TANZANIA FEKI?


JAMANI HIVI WATANZANIA TUTAACHA LINI KUWA MATAPELI???HUYO DADA "MAGGIE R  MUNTHALI" AMEVAA MISS TANZANIA JE MNAMTAMBUA KWAMBA ALIKUWA MISS TANZANIA MWAKA GANI?AU ALISHIRIKI KATIKA MASHINDANO GANI YA KUMTAFUTA MWAKILISHI WA TANZANIA?SISI KAMA WATANZANIA TUMESIKITISHWA SANA NA KUTAPELIWA HUKU.
TUMESAHAU KUWA ULIMWENGU HUU WA MITANDAO UONGO UONEKANA MARA MOJA.DADA HUYU ALIONEKANA JUMAMOSI WASHINGTON DC KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS AFRICA USA.WASHIRIKI WOTE WALIOSHIRIKI NI WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI KATIKA NCHI ZAO WALIZOTOKA....AU WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI NDANI YA USA YA KUZIWAKILISHA NCHI ZAO.SASA HUYO DADA HAJAWAHI KUSHIRIKI MISS TANZANIA NA KUSHINDA KULE TANZANIA WALA HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA NDANI YA USA...JE IMEKUWAJE AMEVAA UMISS TANZANIA NAKUIWAKILIKSHA TANZANIA JE HASHIM LUNDENGA ANAELEWA SWALA HILI?..JE LUNDENGA ALIMRUHUSU HUYU DADA KUIWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI?..KAMA ALIMRUHUSU ALITUMIA VIGEZO GANI KUMCHAGUA?..TUNAPENDA KUWAKIRISHA NA TUNAMSAPOTI MTANZANIA YEYOTE ANAYETUWAKIRISHA NJE YA NCHI LAKINI APITIE KATIKA NJIA ZILIZO SAHIHI SIO KUGUSHI KUJIITA MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA KUTAFUTA MISS TANZANIA NDANI NA NJE YA NCHI?...KAMA TUMEKOSEA ALIISHA WAHI BASI BWANA LUNDENGA TUNAOMBA PICHA ZAKE AKIWA KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA POPOTE PALE NDANI NA NJE....
NA TUNAOMBA UTWAMBIE JE ALISHINDA NA KUTWAA TAJI HILO?.....WAPO MAMISS WENGI AMBAO WANAFANYA KAZI KUBWA SANA KUWEZA KUFIKIA KUITWA MISS,WAMEVIJA JASHO KUPITIA VIKWAZO HADI KUSHINDA NA KUIWAKIRISHA NCHI VYEMA....TUNAOMBA MTU ANAPOAMUA KUIBEBA BENDERA YA NCHI ASIWE MTU WA KUFOJI.....HUU NI WIZI WA KUMUITA MTU MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUWA..TUNAOMBA PIA SWALA HILI MHESHIMIWA LUNDENGA KAMA SIO LA HALALI BASI LIFIKISHWE KWA WAANDALIZI WA MISS AFRICA USA KWANI INAWEZEKANA KABISA WAMERUBUNIWA..AU LABDA WANAVIGEZO VYAO.TUNAOMBA WATANZANIA MLIOKO NJE YA NCHI MSITUDANGANYE NA KUTUIBIA KWANI WATANZANIA SIKUIZI TUKO KWENYE MITANDAO....HABARI HIIZI PIA TUTAZIPELEKA WIZARA YA MABO YA NJE KWANI HUWEZI KUIWAKIRISHA NCHI PASIPO HALALI..!
AHSANTE.....MUNGU IBARIKI TANZANIA !

WADAU WASHINGTON
¤¤¤¤¤¤¤¤ 

MAJIBU YAO HAYOO

WADAU WA UREMBO WASHINGTON DC USA, MAGGIE MUNTHALI ANAHAKI YA KUSHIRIKI KAMA MTANZANIA



Na Father Kidevu Blog, 

KAMATI ya Miss Tanzania imesema kuwa Mrembo Maggie Munthali hana pingamizi lolote katika kushiriki mashindano hayo kwa kutumia jina la Tanzania na badala yake  kufanya hivyo anatumia uzalendo wake kuitangaza nchi Kimataifa.

Ufafanuzi huo umekuja kufuatia malamiko yaliyotolewa na baadhi ya wadau wa Urembo hasa Watanzania waishio katika jiji la Washingtoni DC, Marekani juu ya Uhalali wa Mrembo Maggie Munthali kuvaa beji ya Miss Tanzania katika mashindano ya kumsaka Miss Afrika USA 2012.

Akizungumza na Blogu hii Msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco amesema kuwa Kamati ya Miss Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano hayo, kwani shindano hilo linawahusu warembo waishio huko lakini wanatoka Tanzania.

Awali akitoa historia ya Mrembo huyo, Rico alisema kuwa Kamati inamfahamu vyema mrembo Maggie Munthali kwani aliwahi kushiriki mashindano hayo ngazi ya Vitongoji na kuishia ngazi ya kanda.

Tumesoma maoni yenu kupitia mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki shindano la urembo la Miss Africa USA.

“Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.” Alisema Ricco.

Pia aliendelea kwa kusema kuwa Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA ILALA  kwa mwaka huo.

Mrembo huyo hakupata nafasi  ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.

Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.

Ricco amesema Kamati ya Miss Tanzania haijui ni vigezo vipi vinatumika katika shindano hilo, na maamuzi yakumpa jina Miss Tanzania na Kamati inaamini kuwa ni mrembo anayewakilisha Tanzania  japokuwa hakuingia  katika Fainali za Taifa.

Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.
 
Father Kidevu Blog ilifanikiwa kufanya utafiti juu ya washiriki wa shindano hilo na kubaini kuwa sio Mamiss halisi wa nchi walizotoka kwani baadhi ya nchi walikuwa zaidi ya mmoja kama vile Kenya. 
Pia baadhi yao Umri unaonesha dhahiri kuwa umekwenda sana kwani washiriki wanapoaswa kuana miaka kuanzia 18 lakini isizidi 29 na hawaendani na vigezo halali vya mashindano ya Urembo yanayofanyika kila mwaka katika nchi husika kwaajili ya kushiriki Miss World.
  
Haya ni baadhi ya Masharti na Vigezo vya Mshiriki ambayo yapo katika mtandao huu   http://www.missafricaunitedstates.com/application/registration/


ELIGIBILITY

1.Applicant must have at least one parent from an African country.
2. An applicant with parents from two countries will choose to represent only one country of her choice.
3. Applicants must be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to compete in.
4.Applicants above 29 years of age will not be accepted
5.We accept Applications from students, professionals and girls wishing to develop themselves and improve their status.
6. Applicants are strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to uplift the community in need.
7. No Pageant Experience is required.
8. Applicants must be female at birth and never married.
 

DIAMOND PLATNUMZ: NATAKA KULEWA OFFICIAL VIDEO

Sunday, 2 December 2012

SHOW YA JB MPIANA BONGO ILIVYOFANA LICHA YA KUTOKEA HITILAFU YA UMEME





 JB Mpiana akiingia katika viwanja vya Leaders Club jana usiku mida ya saa tisa kasoro, kuanza shoo baada ya kuchelewa kupanda kutokana na umeme kuzingua, huku bendi ya Mashujaa ikishindwa kuzindua rasmi, albam yake ya Risasi Kidole. Picha Zote na mtandao wa www.sufianimafoto.blogspot.com
 JB Mpiana, akipanda jukwaani kuanza kushambulia jukwaa.
 Jb Mpiana, akianza kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi viwanjani hapo, akiwa na wanenguaji wake.
 Mashabiki wakishangilia na kupata kumbukumbu kupitia simu zao za mkononi.
 Sebene lilianza kuchanganya kama hivi.....huku Rapa wa bendi hiyo akikamua.....
 Rapa wa bendi hiyo akiwangoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa.
 Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa, Chalz Baba, akiingia uwanjani hapo akiwa na Trekta, ikiwa ni staili yake ya kuingia ukumbini hapo, ambayo hata hivyo alishindwa kulitumia Trekta hilo kuwaonyesha mashabiki wake, kutokana na kuzinguliwa na umeme.
 Chalz Baba, akishuka katika Trekta lake kuingia katika shoo hiyo.
 Mtangzaji wa EATV, Patrick Nyembela, akiwa na wadau wakifuatili uzinduzi huo...
 William Malecela (kushoto) akiwa na Juma Pinto (katikati) na Ben Kisaka, wakiwasili katika uzinduzi huo.
 Njiwa naye alikuwapo kufikisha salam za uzinduazi huo.
 Wanenguaji wa Mashujaa Band, wakikamua jukwaani wakati wa shoo ya ufunguzi wa uzinduzi wa albam yao, ambao shoo hii waliicheza jukwaani bila kumalizika kutokana na matatizo ya umeme.
 'Mkaanga Chips' wa Mashujaa, akizicharaza Drams.
 Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiingia kwa staili yao ya kucheza muziki wa Kihindi, wakati wa shoo yao ya pamoja, ambayo hata hivyo haikuweza kumalizika.
 Wanenguaji wa Mashujaa, wakikamua jukwaani..
 Makamuzi yakiendelea..
 Shoo ilikuwa ni tamu kwa kweli, lakini haikuwa na raha kutokana na karaha ya umeme.
 Mpiga Tumba wa bendi hiyo, MCD, akizicharaza tumba....
 Sehemu ya mashabiki wa VIP waliolipa kiingilio cha Sh. 100, 000 kila mmoja, wakiwa katika eneo lao la VIP.
 Gari, alilotumia JB Mpiana kuingia uwanjani hapo......
 Mafundi mitambo, wakishangaa wasijue la kufanya baada ya kukatika kwa umeme huo kila muda.
 Mtangazaji Ben Kinyaiya, akifanya mahojiano na Jado Fidifosi wakati wakiendelea kulazimisha shoo hiyo.
 Ben Kinyaiya naye akisebeneka..
 Mnenguaji wa Mashujaa, akikamua.
 Rapa wa Bendi ya Mashujaa, Ferguson, akiwachezesha wanenguaji wake.....kwa rap ya 'Kibega'
 Ni Nyuzi bin Nyuzi hapa.......
 Mafundi wakihaha kurekebisha Jenereta baada ya kuzingua.......
 Sehemu ya mashabiki, wakisebeneka.....
 Wanasa matukio nao hawakuwa nyuma katika kazi yao......
 Kazi na dawa, Paparazi huyu baada ya kuchenguka vilivyo na sebene la JB, ilibidi kusahau kazi na kuamua kusebeneka.
 VIP.......
 Wanasa matuakaio wakiwa kazini, (katikati) ni Meneja wa Mtandao wa Sufianimafoto, akiwa kazini.
 Huyu naye alinaswa na kamera ya Sufianimafoto, si mwingine bali ni mzee wa Mtaa kwa Mtaa Blog, Othman Michuzi, akisebeneka.
 Mkaanga chips wa JB, akizicharaza Drams.....

BENDI ya Wenge BCBG usiku wa kuamkia leo ilikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliofika kwenye viwanja vya Leaders Club kushuhudia uzinduzi wa albam ya pili ya Bendi ya Mashujaa ya Risasi Kidole, huku matatizo ya kiufundi yakisababisha bendi ya Mashujaa kushindwa kuzindua albamu hiyo.
Pamoja na kuchelewa kuanza kwa shoo hiyo, kutokana na matatizo ya kukatika kwa umeme kila muda, JB Mpiana alianza kuwatanguliza wanamuziki wake wakiongozwa na mmoja wa waanzilishi wa bendi hiyo, Shai Ngenge, na kupiga sebene kabambe kabla ya kufuatiwa na wimbo wa zamani wa Kinie  Bouger,  ambao enzi zake alishirikiana na akina, Ngiana Makanda, miaka ya katikati ya 1990.
Wimbo huo uliweza kuondoa kero kwa mashabiki hao na kuwasahaulisha yale yaliyokuwa yakiwatokea wanamuziki wa Mashujaa, ambao kila walipokuwa wakipanda jukwaani na wanapofika kuanza sebene umeme unakatika, jambo lililowafanya kupanda jukwaani mara nne, lakini wakishindwa kumaliza wibo mmoja tu wa Risasi Kidole.
JB Mpiana alionekana kuwa ni mkombozi kwa mashabiki wachache waliokuwa wamebaki huku wakipiga moyo konde kuwa hawataondoka viwanjani hapo bila ya kumuona JB, katika uzinduzi huo kutokana na burudani safi.
Kitu ambacho kiliwashangaza mashabiki wengi ni kutokatika kwa mara kwa mara kwa umeme kama ilivyotokea kwa bendi ya Mashujaa ilipokuwa jukwaani.  Mpiana aliweza kufanya kweli katika shoo hiyo kwani umeme haukukatika mpaka aliposhuka jukwaani majira ya saa 10 alfajiri.

Katika shoo hiyo, Mpiana aliweza kupiga nyimbo mbali mbali za zamani ikiwa pamoja na Barakuda, Djodjo Ngonda, Walay Danico, Dizo Dizo na zile mpya katika mtindo wa non-stop.
Mashujaa ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na mara walipoanza kucheza shoo ya ufunguzi ambao imewajumuisha wanenguaji wa kike na wa kiume na waimbaji, umeme ulikatika na kazi ya kuanza kurejesha ikaanza na kuchukua muda wa dakika zisizopungua 30.
Tatizo hilo liliendelea mara kwa mara huku bendi hiyo ilishindwa kumaliza tatizo hilo na jitihada za kutatua hazikutoa jibu la mara moja, huku Mmoja wa viongozi wa Bendi hiyo, King Dodoo, akionekana kuhaha kila kona ya uwanja huo akiwa na Babu aliyekuwa akijitahidi kusoma dua ili Jenereta hilo liweze kufanya kazi bila kusumbua.
 Mafundi walijitahidi sana na mara baada ya mashabiki kutaka JB Mpiana apande, mafundi walitatua tatizo hilo na kumwezesha mwanamuziki huyo kufanya shoo bila tatizo hadi alipomaliza ratiba yake.
Katika tukio jingine lililojitokeza viwanjani hapo ni Mkurugenzi wa bendi hiyo, Mama Sakina, aliyeanguka ghafla, ikieleza ni presha ya ghafla kutokana na kile kilchokuwa kikiendelea mahala hapo na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.