Tuesday, 4 December 2012

NGWASUMA-VUTA NIKUVUTE TUVUTANE,BURULA NIKUBURULE TUBURULANE-UJUMBE MKALI SANA HAPAhuwa najisikia raha sana mara kwa mara nikisikia nyimbo hii,ujumbe umetulia na kuna ukweli ndani yake,nafurahi siku hii wazee wa ngwasuma wanaimba kiswahili mwanzo mwisho na sie maganga tunaelewa wanachoimba.
na katika hilo ndio nakuja kugundua kwamba hawa jamaa kumbe walikuwa wanapiga nyimbo kali nzito na zenye ujumbe mkali hapo nyuma,sema usipokuwa unaelewa we unasubiri ichanganye ucheze yaishe.
hapa kuna ujumbe ambao mara kwa mara huwa unanirudia akilini.hasa pale wanapoimba kwamba "usilinganishe riziki na uhai wa bin adamu,uhai wa bin adamu ni bora kuliko riziki,ndugu yako anapofanikiwa huanza kumchukia na kujipa uwezo wakudhuru maisha yake" 
na pale Patcho anapoimba
" kupata kwako isiwe sababu ya kunyanyasa wenzio,mafanikio yako isiwe sababu ya kunivurugia ndoa yangu wee,hakuna aliyekamilika duniani,hakuna aliyekamilika sisi wote mareehemu watarajiwa,wako wapi Mwalimu Nyerere na Mobutu Seseseko?itakua sisi wapangaji,hakuna aliyeweza ishi na tamaa,anayetembea kwa miguu ndoto yake kununua baskeli,aliye na baskeli anatamani pikipiki mwenye pikipiki anatamani corolla,kila mwenye corolla anataka vitara,kila mwenye vitara anatamani apate pajero,mwenye pajero anatamani VX,kila mwenye VX anataka apate Hummer kila mwenye Hummer atatamani ......"and so on
" and on.

mashairi hayajaishia hapo kuna Kabeza anampokea Patcho na yeye anaimba yake ingawa siku hizi hayuko vizuri upstair kwa ajili ya hao hao bin adamu wamemtengeneza lakini kumwaga mashairi kama kawaida.

acha pale mwisho ikichanganya unapokuja kumsikia Kitokololo"kuku" na G7 wanapokucheza tingisha tingisha mayemba,inauma inai.... na mwisho utamu wa vanilla eeeh na nzombo na matembele.raha tupu

TUPENDANE WAJAMAA WENZANGU,SIE WAPANGAJI TU HAPA DUNIANI HASA SVERIGE..

No comments:

Post a Comment