Monday 17 December 2012

koffi Olomide awachengua vilivyo mashabiki wa MWANZA

Kofii Olomide na Mwimbaji Cindy wakiimba huku wakiwa amezungukwa na wanenguaji wake
Mwanamuziki Kofii Olomide akipanda jukwaani huku akisinddikizwa na waimbaji wake.
Cindy katikati Mwimbaji mahili wa kike wa mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani kalba ya Kofii Olomide mwenyewe kupanda jukwaani.
Kazi iko hapa kama wanavyoonekana wanenguaji hao wakicheza kwa sataili ya aina yake.
Hii ilichezwa kwa kwenda mbele na kurudi nyuma huku wakiwa wameshikana.
Palikuwa hapatoshi kwa shoo kabambe kabisa kutoka kwa wanenguaji wa Kofii Olomide.
Ili mradi burudani iliyopangika kutoka kwa wanenguaji hao
Staili hiyo ilichezwa kwa hisia pia
Kutoka kulia ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa  (SBL), Anitha Msangi Maurice Njowoka na Patrick Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakishoo love kwa picha.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru kulia na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakiwa katika picha ya pamoja
Wadau kutoka Miss Tanzania wakiwa katika onesho hilo.
 
Rachel wa THT akicheza na mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide.
 
Kofii Olomide akimpongeza msanii Rachel wa THT baada ya kuonyesha uwezo wake katika kuimba kwenye onesho hilo.
 
Waimbaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakiimba kwa hisia katika enesho hilo.
 
Rapa wa mwanamuziki Kofii Olomide anayejulikana kwa jina la Computar akighani huku wanenguaji wa kiume wakiingia jukwaani.
 
Jukwaani ni Recho wa kundi la  THT kutoka jijini Dar es salaam akinendelea kutoa burudani jukwaani
 
H. Baba akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wa jijini Mwanza wakati akitoa burudani ya utangulizi kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide Kupanda jukwaani.
 
Pepe Kale wa Mwanza naye akafanya mambo makubwa na kukubalika na umati wa mashabiki waliohudhuria katika onesho hilo.
 
Wasanii wa Kundi la THT wakitumbuiza katika onesho hilo.
 
Bendi ya Hill Way ya Mwanza ikitumbuiza katika utangulizi
 
Kundi la Hill Way Band likifanya vitu vyake jukwaani katika utangulizi wa burudani za tamasha la Tusker Carnival kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide kupanda jukwaani.
Mashabiki wakiwa wameanza kumiminika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
Mashabiki wakiwa  kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakisubiri kuona burudani ya Kofii Olomide.
 
Haya ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kujipatia bia yako ya Tusker Lager na vinywaji vingine vinavyotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
 
Haya ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kujipatia bia yako ya Tusker Lager na vinywaji vingine vinavyotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti

No comments:

Post a Comment