Friday, 14 December 2012

KOFFI OLOMIDE TAYARI KWA MAKAMUZI BONGO HAPO KESHO

 
 
 Mwanamuziki  Kofii Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo kwenye hoteli ya serena Dar es salaam, wakati alipozungumzia onesho lake linalotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Leaders kesho jumamosi, ikiwa ni kuadhimsha shamrashamra za sikukuu kwa maonyesho kabambe yatakayofanyika Jijini Dar es salaam, Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba,  maonyesho hayo yanadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Tusker Lager yakipewa jina laTUSKER CARNIVALS CELEBRATIONS FEATURING KOFFI OLOMIDE!
Mwanamuziki huyo amesema ili kuwa mwanamuziki mzuri Tanzania ni nchi nzuri na muhimu kwa wanamuziki katika kujipima ili kujua kuwa ni mwanamuziki wa kiwango gani. Akaongeza kwa kusema “Namshukuru Rafiki yangu mkubwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga kwa kunifanya niwe tajiri hivyo naipenda sana Tanzania ni  nchi Muhimu kwangu” akamaliza Kofii Olomide
Baada ya onesho la Leaders Kesho mwanamuziki Kofii Olomide jumapili atafanya onesho lingine jijini Mwanza, ambako wakazi wa Mwanza watapata burudani ya mwanamuziki huyo Gwiji wa muziki Afrika
 
 
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Ganon akizungumza katika mkutano huo na kukaribisha ujio wa maonyesho hayo ambayo yatawapa burudani wananchi hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismass.
 
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Group Bw Joseph Kussaga akimkaribisha mwanamuziki Kofii Olomide ili kuongea na waandishi wa habari kuhusu maonyesho yake hayo yatakayofanyika jijini Dar es salaam na Mwanza.
 
 
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru akizungumzia mipango na utaratibu mzima wa maonesho ya mwanamuziki Kofii Olomide na jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kuwapa mashabiki  Burudani bora kabisa kupitia bia yake ya Tusker Lager.
 
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Nandi Mwiyombela akimkaribisha mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Bw Ephraim Mafuru ili kuongea na wanahabari katika mkutano huo.
 
 
Mwanamuziki Kofii Olomide akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon mara baada ya kuwasili katika chumba cha mkutano leo, Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw. Ephraim Mafuru. 
 
Mwanamuziki Kofii Olomide akisalimiana na Mkurugenzi  wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru mara baada ya kuwasili kwenye chumba cha mkutano na waandishi wa habari leo, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon.
 
 
Mwanamuziki Kofii Olomide akisaini katika bango maalum linalowahimiza watu kuacha kuendesha huku wakiwa wamelewa pombe katika kampeni ya kupunguza ajali barabarani ya Kunywa Pombe Kistaarabu inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa wateja wake, anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon.
Kutoka 
 
kulia katika picha ni Anitha Msangi Meneja Msoko wa Tusker Lager, Maurice  Njowoka Meneja wa Kinywaji cha Tusker, Sialouise Shayo Brand Executive na Agnes Kiondo kutoka Serengeti wakiwa katikia mkutano huo.
Kutoka 
 
kulia ni Steve Gannon Mkurugenzi Mtendaji SBL, Ephraim Mfuru Mkurugenzi wa Masoko SBL na Nandi Mwiyombela Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano SBL wakimuangalia kwa makini mwanamuziki Kofii Olimide wakati akiongea na wanahabari.
 
 
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwasili katika chumba cha mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon na kushoto na Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga wakifuatana naye.
 
 
Chanzo:fullshangweblog

No comments:

Post a Comment