Monday 3 December 2012

WABONGO NA FITNA FITNA!

SOMA HAPO


                                      MISS TANZANIA FEKI?


JAMANI HIVI WATANZANIA TUTAACHA LINI KUWA MATAPELI???HUYO DADA "MAGGIE R  MUNTHALI" AMEVAA MISS TANZANIA JE MNAMTAMBUA KWAMBA ALIKUWA MISS TANZANIA MWAKA GANI?AU ALISHIRIKI KATIKA MASHINDANO GANI YA KUMTAFUTA MWAKILISHI WA TANZANIA?SISI KAMA WATANZANIA TUMESIKITISHWA SANA NA KUTAPELIWA HUKU.
TUMESAHAU KUWA ULIMWENGU HUU WA MITANDAO UONGO UONEKANA MARA MOJA.DADA HUYU ALIONEKANA JUMAMOSI WASHINGTON DC KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS AFRICA USA.WASHIRIKI WOTE WALIOSHIRIKI NI WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI KATIKA NCHI ZAO WALIZOTOKA....AU WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI NDANI YA USA YA KUZIWAKILISHA NCHI ZAO.SASA HUYO DADA HAJAWAHI KUSHIRIKI MISS TANZANIA NA KUSHINDA KULE TANZANIA WALA HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA NDANI YA USA...JE IMEKUWAJE AMEVAA UMISS TANZANIA NAKUIWAKILIKSHA TANZANIA JE HASHIM LUNDENGA ANAELEWA SWALA HILI?..JE LUNDENGA ALIMRUHUSU HUYU DADA KUIWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI?..KAMA ALIMRUHUSU ALITUMIA VIGEZO GANI KUMCHAGUA?..TUNAPENDA KUWAKIRISHA NA TUNAMSAPOTI MTANZANIA YEYOTE ANAYETUWAKIRISHA NJE YA NCHI LAKINI APITIE KATIKA NJIA ZILIZO SAHIHI SIO KUGUSHI KUJIITA MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA KUTAFUTA MISS TANZANIA NDANI NA NJE YA NCHI?...KAMA TUMEKOSEA ALIISHA WAHI BASI BWANA LUNDENGA TUNAOMBA PICHA ZAKE AKIWA KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA POPOTE PALE NDANI NA NJE....
NA TUNAOMBA UTWAMBIE JE ALISHINDA NA KUTWAA TAJI HILO?.....WAPO MAMISS WENGI AMBAO WANAFANYA KAZI KUBWA SANA KUWEZA KUFIKIA KUITWA MISS,WAMEVIJA JASHO KUPITIA VIKWAZO HADI KUSHINDA NA KUIWAKIRISHA NCHI VYEMA....TUNAOMBA MTU ANAPOAMUA KUIBEBA BENDERA YA NCHI ASIWE MTU WA KUFOJI.....HUU NI WIZI WA KUMUITA MTU MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUWA..TUNAOMBA PIA SWALA HILI MHESHIMIWA LUNDENGA KAMA SIO LA HALALI BASI LIFIKISHWE KWA WAANDALIZI WA MISS AFRICA USA KWANI INAWEZEKANA KABISA WAMERUBUNIWA..AU LABDA WANAVIGEZO VYAO.TUNAOMBA WATANZANIA MLIOKO NJE YA NCHI MSITUDANGANYE NA KUTUIBIA KWANI WATANZANIA SIKUIZI TUKO KWENYE MITANDAO....HABARI HIIZI PIA TUTAZIPELEKA WIZARA YA MABO YA NJE KWANI HUWEZI KUIWAKIRISHA NCHI PASIPO HALALI..!
AHSANTE.....MUNGU IBARIKI TANZANIA !

WADAU WASHINGTON
¤¤¤¤¤¤¤¤ 

MAJIBU YAO HAYOO

WADAU WA UREMBO WASHINGTON DC USA, MAGGIE MUNTHALI ANAHAKI YA KUSHIRIKI KAMA MTANZANIA



Na Father Kidevu Blog, 

KAMATI ya Miss Tanzania imesema kuwa Mrembo Maggie Munthali hana pingamizi lolote katika kushiriki mashindano hayo kwa kutumia jina la Tanzania na badala yake  kufanya hivyo anatumia uzalendo wake kuitangaza nchi Kimataifa.

Ufafanuzi huo umekuja kufuatia malamiko yaliyotolewa na baadhi ya wadau wa Urembo hasa Watanzania waishio katika jiji la Washingtoni DC, Marekani juu ya Uhalali wa Mrembo Maggie Munthali kuvaa beji ya Miss Tanzania katika mashindano ya kumsaka Miss Afrika USA 2012.

Akizungumza na Blogu hii Msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco amesema kuwa Kamati ya Miss Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano hayo, kwani shindano hilo linawahusu warembo waishio huko lakini wanatoka Tanzania.

Awali akitoa historia ya Mrembo huyo, Rico alisema kuwa Kamati inamfahamu vyema mrembo Maggie Munthali kwani aliwahi kushiriki mashindano hayo ngazi ya Vitongoji na kuishia ngazi ya kanda.

Tumesoma maoni yenu kupitia mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki shindano la urembo la Miss Africa USA.

“Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.” Alisema Ricco.

Pia aliendelea kwa kusema kuwa Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA ILALA  kwa mwaka huo.

Mrembo huyo hakupata nafasi  ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.

Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.

Ricco amesema Kamati ya Miss Tanzania haijui ni vigezo vipi vinatumika katika shindano hilo, na maamuzi yakumpa jina Miss Tanzania na Kamati inaamini kuwa ni mrembo anayewakilisha Tanzania  japokuwa hakuingia  katika Fainali za Taifa.

Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.
 
Father Kidevu Blog ilifanikiwa kufanya utafiti juu ya washiriki wa shindano hilo na kubaini kuwa sio Mamiss halisi wa nchi walizotoka kwani baadhi ya nchi walikuwa zaidi ya mmoja kama vile Kenya. 
Pia baadhi yao Umri unaonesha dhahiri kuwa umekwenda sana kwani washiriki wanapoaswa kuana miaka kuanzia 18 lakini isizidi 29 na hawaendani na vigezo halali vya mashindano ya Urembo yanayofanyika kila mwaka katika nchi husika kwaajili ya kushiriki Miss World.
  
Haya ni baadhi ya Masharti na Vigezo vya Mshiriki ambayo yapo katika mtandao huu   http://www.missafricaunitedstates.com/application/registration/


ELIGIBILITY

1.Applicant must have at least one parent from an African country.
2. An applicant with parents from two countries will choose to represent only one country of her choice.
3. Applicants must be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to compete in.
4.Applicants above 29 years of age will not be accepted
5.We accept Applications from students, professionals and girls wishing to develop themselves and improve their status.
6. Applicants are strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to uplift the community in need.
7. No Pageant Experience is required.
8. Applicants must be female at birth and never married.
 

No comments:

Post a Comment