Sunday, 16 December 2012

koffi Olomide awakuna wakazi wa jiji la Dar


 Mwanamuziki mahiri ndani ya kundi la Quartie Latin aitwae Cindy, linaloongozwa na nyota wa muziki wa dansi kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akiimba jukwaani usiku huu  mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi (hawapo pichani),kwenye tamasha la usiku wa Tusker Carnival ndani ya viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
 Mwanamuziki Koffi Olomide akijimwaya mwaya kwa madaha kabisa jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Tusker Carnival,huku akishangiliwa na umati mkubwa watu uliohudhuria tamasha hilo.

 Pichani juu na chini ni Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide sambamba na skwadi lake la Quartie Latin


Koffi Olomide akimtambulisha rafiki yake mkubwa jukwaani,Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga,ambaye ndiye aliyemleta hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya  bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker,ambapo pia mwanamuziki huyo alimshukuru sana Joseph kusaga kwa ukarimu wake
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,akizungumza machache na kuwashukuru sana wadhamini wa onesho hilo sambamba na wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye onesho hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa.
 

 
Mwanamuziki  Kofii Olomide akiimba jukwaani na kundi lake katika Onesho  linalofanyiki usiku huu  kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo wageni waalikwa na mashabiki mbalimbali wamefurika katika viwanja hivvyo , ili waweze kushuhudia shughuli pevu ya mwanamuziki huyo nguli wa muziki  Barani Afrika.

Fullshangweblog na kikozi kazi chake chote iko katika eneo la tukio ili kukumuvuzishia matukio  yatakayojiri katika viwanja vya Leaders usiku huu moja kwa moja katika kukupasha habari na kukuburudisha pia.
 
Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide akifanya vitu vyake jukwaani kama anavyoonekana katika picha.
  Kofii Olomide akiimba na mmoja wa waimbaji wake Cindy. Mwanamuziki Kofii Olomide  akiwa na mmoja wa waimbaji wake wa kike wakipagawisha mashabiki wa bendi hiyo  waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Leaders ili kushuhudia kile anachokifanya jukwaani.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Group akizungumza kumshukuru mwanamuziki Kofii Olomide na mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika onesho hilo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

 
Vimwana wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakimwaga mauno kwa kwenda mbele jukwaani katika onesho hilo.
 
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa amezungukwa na vimwana hao ambao ni wanenguajia wa bendi yake huku akiwa katikati yao kama mfalme.
 
Hapa ni Burudani ya mauno tu kama inavyoonekana madau.
 
Mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki Kofii Olomide wakifuatilia kwa makini wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
 
Mashabiki wa mwanamziki Kofii Olomide wakishangilia kwa furaha wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
pica na habari kwa hisani ya kifna jiachie blog

No comments:

Post a Comment